MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO MTUME (ABU TALIB)
KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
![]()
![]()
KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO
Baada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Kiongozi ambaye alikabidhiwa mamlaka ya kukichimba upya kisima cha zamzam baada ya kufukiwa na watu kutoka kabila la Jurhum pindi walipoondoka Makkah. Alisimama Abu Talib kumlea mtoto wa ndugu yake. Kwani huyu ndiye aliyekuwa mtoto mkybwa wa Abdul al-Muttalib.
Abu Talib alimpenda sana kijana wake zaidi ya anavyowapenda watoto wake. Mtume (s.a.w) alikuwa ni mwenyekuridhika kwa kile ambacho alikuwa akikipata. Allah alimuongezea rizk mzee Abu Talib. Mzee huyu alimlea kijana wake Mpaka alipofika umri wa miaka arobaini. Watu walimpenda kijana Muhammad jinsi alivyokuwa na tabia njema na uaminifu.
Watu wa Makkah walikuwa wakiomba mvua kupitia utukufu wake. Imesimuliwa kutoka kwa Ibn โAsakir kuwa Jalhamah bin Arfuta kuwa amesema nilifika Makkah wakati ambao kulikuwa hakuna mvua, Maquraish wakatoka kumueleza mzee Abu Talib kuwa awaombee mvua. Basi akatoka akiwa na kijana chake na akamsimamisha pembeni ya ukuta wa al-kabah kisha akaomba dua. Kwa hakika kulikuwa hakuna mawingu lakini ghafla mawingu yakajikusanya kutoka huku na kule na hatimaye mvua ikanyesha
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Bongolite - Game zone - Play free game ๐2 Kitau cha Fiqh ๐3 ai web app ๐4 Simulizi za Hadithi Audio ๐5 web hosting ๐6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Kuangamia kwa Mtoto na Mke wa Nuhu(a.s)
Tukirejea Qurโan (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.
Soma Zaidi...Vipengele vya Mikataba ya โAqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina
Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ismail(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a.
Soma Zaidi...Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)
Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a.
Soma Zaidi...