7.1 Hali ya Bara Arab zama za Jahiliyyah.
Jiografia ya Bara Arab.
- Bara Arabu imezungukwa na bahari katika tatu, Magharibi kuna bahari ya Shamu,
Mashariki kuna Ghuba ya Uajemi na Oman, Kusini kuna bahari ya Uarabuni na
Kaskazini ni Jangwa la Syria.
- Bara Arabu liko kati kati ya mabara matatu; Asia, Ulaya na Afrika.
- Saudi Arabia ndio nchi kubwa kuliko zote Bara Arabu ambamo kuna miji mitakatifu
ya Makkah na Madinah.
?Hali ya Maadili na ushirikina katika jamii wakati wa kuzaliwa Mtume (s.a.w).
- Wakati anazaliwa Mtume mwaka 570 A.D (karne ya 6 A.D) dunia nzima ilikuwa
katika giza totoro la ujahili.
- Maisha ya jamii yalikuwa yanaendeshwa kibabe na kibinafsi kwa kufuata matashi
ya nafsi zao.
- Ubabe, ukandamizaji, unyonyaji, uporaji na dhuluma katika maisha yalionekana
kama matendo ya kishujaa na kujivunia.
- Walizama katika ushirikina kiasi cha watu kuweza kutembea na miungu mifukoni
mwao.
- Hali hii ya giza totoro ilienea pia nchi na mabara mbali mbali ulimwenguni kote.
- Dini kubwa zilizokuwepo muda huo zilikuwa ni Uyahudi na Ukristo lakini
hazikuweza kumkomboa mwanaadamu kwa lolote hata kidogo.
- Hapakuwa na serikali, kila kabila lilikuwa na kiongozi na taratibu zake katika
kuendeshea maisha.
- Unyanyasaji wa wanawake kila nyanja, mauwaji ya watoto wa kike wakiwa hai
ilikuwa ni desturi ya kawaida katika maisha ya jamii ya Waarabu.
Mji wa Makkah na Kabila la Kiqureish.
- Mji wa Makkah ni mji mkongwe wa kihistoria ulioanzishwa na Nabii Ibrahiim miaka mingi iliyopita.
- Nabii Ibrahim (a.s) na mwanae Nabii Ismail (a.s) ndio walioinua kuta za nyumba tukufu ya Ka’abah kwa amri ya Allah (s.w).
Rejea Qur’an (2:127).
- Ka’abah ni nyumba ya mwanzo na pekee ulimwenguni iliyowekwa kwa ya kuhiji wanaadamu wote ulimwenguni.
Rejea Qur’an (22:27), (3:96) na (22:29).
- Kutokana na jangwa na ukame wa mji huu, Allah (s.w) alijaalia chem.-chem ya maji ya zamzam kutokana dua ya Nabii Ibrahim (a.s).
Rejea Qur’an (14:37).
- Mji huu ulipata utukufu kutokana na uwepo wa nyumba tukufu ya Ka’aba ambapo kabila la Qureish ndio walikuwa walinzi wa nyumba hiyo.
Rejea Qur’an (106:1-4).
- Ni mji alikozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w) mwaka 570 A.D katika kabila la Kiqureish mwaka wa ndovu.
Rejea Qur’an (105:1-5).
- Kabila la Kiqureish liliheshimika kuliko makabila mengine kwa huduma walizokuwa wakitoa kwa watu wanaohiji, misafara ya biashara na kule kuitumikia nyumba hiyo.
- Kabila la Qureish ni miongoni mwa makabila ya waarabu yaliyojishughulisha sana na biashara mbali mbali ndani na nje ya Makkah kwa muda mrefu.