SURA YA SITA
HUKUMU ZA QALQALA
QALQALAH – KUGONGA
Katika hukmu ya Tajwiyd, ni mgongano wa kutetema unaosababishwa na herufi maalum za qalqalah zinapokuwa na sukuwn1, aidha iwe ya asili au ya kuzuka kwa ajili ya kusimama. Herufi za qalqala ni قُ طْ بُ جَ دّ.
Qalqalah inagawanyika katika daraja mbili:
الْقَلْقَلَةُ الْكُبْرى . 1 Al-Qalqalatul-Kubraa -Qalqalah Kubwa Inapokuwa herufi ya qalqalah mwisho wa neno lenye kusimamiwa.
الْقَلْقَلَةُ الصُّغْرى . 2 - Al-Qalqalatus-Sughraa - Qalqalah Ndogo Inapokuwa herufi ya qalqalah katikati ya neno au mwisho wa neno lakini si neno lenye kusimamiwa.