picha

Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu

Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu

(viii)Dai la Kurekebisha Tabia ya Waarabu:



Miongoni mwa wale wanaosema kuwa Muhammad (s.a.w) ndiye aliyetunga Qur-an wapo wanaodai kuwa Muhammad (s.a.w) alifanya hivyo kwa nia nzuri ya kutaka kujenga tabia na mwenendo mzuri miongoni mwa ndugu zake Waarabu. Yaani, Muhammad (s.a.w) alichukizwa sana na tabia mbaya walizokuwa nazo


Waarabu wa zama zake na hivyo akaona lazima ajitahidi kuziondoa. Na ili afanikishe lengo lake hilo akaona atunge Qur-an na asingizie kuwa inatoka kwa Allah (s.w). Dai hili pia halina nguvu kwa sababu zifuatazo:



Kwanza, kujenga mwenendo mzuri wa tabia za watu ni jambo jema ambalo laweza kutekelezwa pasi na kutumia udanganyifu na uovu mwingine. Ni kipi kilichomfanya Muhammad (s.a.w) atumie uwongo na udanganyifu ili awafundishe watu kuwa wa kweli na waaminifu?



Pili, Qur-an imeitaja dhambi ya kuzua uwongo kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa:


"Na nani dhalimu mkubwa kuliko yule amtungiaye uwongo Allah au mwenye kusema: "Nimeletewa wahyi," na hali hakufunuliwa chochote; na yule asemaye: "Nit ateremsha (ufunuo) kama ule aliouteremsha Allah." Na kama ungewaona madhalimu watakapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono yao (na kuwaambia): "Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ifedheheshayo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allah pasipo haki na kwa vile mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Aya zake." (6:93)



Aya hii inasema hakuna dhalimu mkubwa kuliko yule mtu ambaye atamzulia uwongo Allah au atakayesingizia kuwa amepata wahyi kutoka kwa Allah na ilhali hakupata.Halafu aya hii inataja jinsi watu wa aina hiyo watakavyofedheheshwa na jinsi watakavyopapatika wakati wa kutolewa roho zao.



Lau kama Muhammad (s.a.w) angekuwa ndiye aliyeitunga halafu akamsingizia Allah (s.w), asingeiweka aya kama hii katika Qur-an kwa sababu angehisi kuwa anajitukana mwenyewe na kujilaani mwenyewe. Pia kwa kuhofia kuwa yaweza kutokezea siku ambayo watu watamgundua angehakikisha kuwa anaiandika aya hii kwa namna ambayo haitamfedhehesha hapo atakapojulikana.



Angeweza kwa mfano kusema: "Hapana lawama kwa wale ambao, ikiwa hapana budi kusema uwongo kwa ajili ya Allah." St. Paulo kwa mfano ameandika hivi katika Biblia:
Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi." (Warumi 3:7)
Aidha madai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili aitumie katika kurekebisha mwenendo wa tabia za watu pia yanatenguliwa na ukweli kwamba Qur-an haikushuka yote mara moja bali ililetwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka 23. Na katika kipindi hicho Qur-an ilitoa ahadi ya kujibu maswali yote yatakayoulizwa wakati Qur-an bado inashuka.


Na kama mtayauliza, maadam inateremshwa Qur-an mtabainishiwa " (5:101)
Watu waliitumia fursa hiyo iliyotolewa na Qur-an kuuliza maswali mbali mbali kama vile juu ya ulevi, kamari, hedhi, ngawira, roho na hata juu ya watu kama Dhur-qarnain. Katika kuyajibu maswali hayo


Qur-an imetumia msemo "Wanakuuliza juu ya jambo kadhaa. Sema: Lipo namna kadhaa." Kwa mifano halisi tazama Qur-an 2:189, 2:215, 2:217, 2:219, 2:220, 2:222, 5:4, 7:187, 8:1, 17:85, 18:83, 20:105 na 79:42.



Tatizo linalojitokeza hapa ni kwamba Muhammad (s.a.w) asingeweza kujua kuwa maswali aliyowaruhusu watu kuuliza yatakuwa yanahusu marekebisho ya mwenendo na tabia za watu. Kwani inadaiwa kuwa haitakuwa jambo la busara kwa rais anayetaka kuzungumzia hali ya chakula nchini mwake kuwaita waandishi wa habari na kuwaruhusu waulize maswali yoyote yanayowatatiza. Rais huyo atakuwa na hakika gani kuwa watauliza juu ya hali ya chakula na siyo juu ya wafungwa wa kisiasa?




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views 1734

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 ai web app     πŸ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰5 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰6 web hosting    

Post zinazofanana:

Sababu za kushuka surat al adiyat

Sura hii iliposhuka ilikuwa kama imekuja kuwasuta Wanafiki waliokuwa wakizungumzahabari za uongo kuhusu jeshi alilolituma Mtume wa Allah.

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA (MIIM SAKINA)

HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA : Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( Ω…Ω’).

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA TAFKHIIM NA TARQIQ

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Quran

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa Surat Al-Asr

Surat Al-Asri imeteremshwa Makka, na hapa utazujuwa sababu za kushuka kwa sura hii

Soma Zaidi...
Ni ipi aya ya mwisho kushuka katika Quran?

Maulamaa katika elimu ya Quran wametofautiana juu ya aya ya mwisho kushuka. Hata hivyo hapa nitakutajia ambayo imependekezwa zaidi

Soma Zaidi...