Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
SURA YA SABA
HUKUMU ZA TAFKHIM NA TARQIQ
AT-TAFKHIYM NA AT-TARQIYQ
1.At-Tarqiyq - Kufanya Nyembamba au Nyepesi
Ni kuitamka herufi kwa kuifanya nyembaba au nyepesi. Hali hii hutokea wakati ulimi uanapokuwa mbali na sakafu la kinywa yaani ulimu unakuwa chini. Tarqiyq hutokea katika herufi za chini yaani إسْتِفال (isfal-herufi za kuinamisha) isipokuwa isipokuwa herufi mbili ر na ل.
2.At-Tafkhiym - Kufanya Nene Au Nzito
Hutokea pale inapotamkwa herufi kwa kuifanya kuwa nene au nzito. Hukumu hii hutokea kwa zile hurufi za اٌلإسْتِعْلاء al-isti’ala yaani herufi za kupanda. Herufi hizi hutamkwa wakati ulimu unapokuwa juu ya sakafu la kinywa.
3.Baina ya Tafkhiym na Tarqiyq
Kuna baadhi ya herufi zinaweza kubeba hukumu zote mbili zilizotajwa hapo juu. Yaani wakati mwingine huwa taeqitq na wakati mwingine huwa tafkheem. Herufi hizo ni kama;-
i) Alif ( ا ) ya madd
ii) Laam ( ل ) ya Lafdhw Al-Jalaalah ( (لله
iii) Raa ( ر)
Laam ( ل ) ya Lafdhw Al-Jalaalah
Kawaida herufi ya ل ni nyepesi ila inapotokea katika jina la Allaah ( ,(سبحانه وتعالى hapo huwa ima ni tafkhiym au tarqiyq kutegemea na i’raab inayotangulia. Ikiwa jina la Allaah ( سبحانه وتعالى ) Limetanguliwa na herufi ya kasrah au ي (yaa) saakinah, hutamkwa kwa tarqiyq. Ama jina la Allaah ( (سبحانه وتعالى Linapotanguliwa na fat-hah, dhwammah au و (waaw) saakinah linatamkwa kwa tafkhiym.
At-Tafkhiym na At-Tarqiyq katika ( ر ) Raa
Halikadhalika herufi hii raa inaweza kuwa nzito au nyepesi, nene au nyembamba kulingana na kanuni za tajweed. Hivyo basi itakuwa tafkhiym katika hali zifuatazo;-
1.itakapokuwa ina fataha au dhummah
2.Inakapokuwa na sakinah na nyuma yake kuna herufi yenye fataha au dhumah
3.Itakapokuwa na sakinah na nyuma yake kukawa na kasra na mbele yake kukawa na herufi za isti’laa
4.Itakapokuwa ina sakina na nyuma yake kukawa na hamzatul-waswl yaani hamza ya kuungia.
5.Itakaposimamiwa kwa sakina halafu nyuma yake kukawa na sakina na nyuma ya hiyo sakina kukawa na fataha au dhumah.
Pia itakuwa nyepezi au nyembaba itakapokutana na hali zifuatazo;-
1.itakapokuwa na kasra
2.Itakapokuwa na sakina na nyuma yake kuna fataha
3.Itakaposimamiwa na sakina na kukawa nyuma yake kuna sakina iliyotanguliwa na kasra.
4.- 5 Inayoitwa الراء الممالة (ar-raa al-mumaalah) ambayo inasomwa kwa vokali ya ‘e’ badala ya kasrah. Hii ni kutokana na riwaayah ya Hafsw ‘an Aaswim. Nayo ni katika neno la pekee katika Qur-aan, na huwa ni ya tarqiyq inapatikana katika surat hud aya ya 41 (11:41)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
(i)Dai kuwa Qur-an ni Mashairi aliyotunga Muhammad (s.
Soma Zaidi...Sura hii ni katika sura za mwisho kushuka, huwendakuwa ndio ya mwisho kabisa. Masahaba waliamini kuwa sura hii imetabiri kifo cha Mtume S.A.W
Soma Zaidi...Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid.
Soma Zaidi...Kusoma Qur'an kuna faida kubwa kwa Muislamu, kwanza kunampatia thawabu, kunatoa nuru maisha yake, mwili wake na kumlinda na mashetani na watu wabaya. Quran ni dawa na pozo kwa magonjwa. Thawabu za Qur-an hulipwa kwa kila herufi. Quran pia huja kutet
Soma Zaidi...