HUKUMU ZA TAFKHIIM NA TARQIQ

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

HUKUMU ZA TAFKHIIM NA TARQIQ

SURA YA SABA
HUKUMU ZA TAFKHIM NA TARQIQ AT-TAFKHIYM NA AT-TARQIYQ
1.At-Tarqiyq - Kufanya Nyembamba au Nyepesi
Ni kuitamka herufi kwa kuifanya nyembaba au nyepesi. Hali hii hutokea wakati ulimi uanapokuwa mbali na sakafu la kinywa yaani ulimu unakuwa chini. Tarqiyq hutokea katika herufi za chini yaani ุฅุณู’ุชููุงู„ (isfal-herufi za kuinamisha) isipokuwa isipokuwa herufi mbili ุฑ na ู„.
2.At-Tafkhiym - Kufanya Nene Au Nzito
Hutokea pale inapotamkwa herufi kwa kuifanya kuwa nene au nzito. Hukumu hii hutokea kwa zile hurufi za ุงูŒู„ุฅุณู’ุชูุนู’ู„ุงุก al-istiโ€™ala yaani herufi za kupanda. Herufi hizi hutamkwa wakati ulimu unapokuwa juu ya sakafu la kinywa.
TAFKHEEM

3.Baina ya Tafkhiym na Tarqiyq
Kuna baadhi ya herufi zinaweza kubeba hukumu zote mbili zilizotajwa hapo juu. Yaani wakati mwingine huwa taeqitq na wakati mwingine huwa tafkheem. Herufi hizo ni kama;-
i) Alif ( ุง ) ya madd
ii) Laam ( ู„ ) ya Lafdhw Al-Jalaalah ( (ู„ู„ู‡
iii) Raa ( ุฑ)
Laam ( ู„ ) ya Lafdhw Al-Jalaalah
Kawaida herufi ya ู„ ni nyepesi ila inapotokea katika jina la Allaah ( ,(ุณุจุญุงู†ู‡ ูˆุชุนุงู„ู‰ hapo huwa ima ni tafkhiym au tarqiyq kutegemea na iโ€™raab inayotangulia. Ikiwa jina la Allaah ( ุณุจุญุงู†ู‡ ูˆุชุนุงู„ู‰ ) Limetanguliwa na herufi ya kasrah au ูŠ (yaa) saakinah, hutamkwa kwa tarqiyq. Ama jina la Allaah ( (ุณุจุญุงู†ู‡ ูˆุชุนุงู„ู‰ Linapotanguliwa na fat-hah, dhwammah au ูˆ (waaw) saakinah linatamkwa kwa tafkhiym.
TAFKHEEM

At-Tafkhiym na At-Tarqiyq katika ( ุฑ ) Raa
Halikadhalika herufi hii raa inaweza kuwa nzito au nyepesi, nene au nyembamba kulingana na kanuni za tajweed. Hivyo basi itakuwa tafkhiym katika hali zifuatazo;-
1.itakapokuwa ina fataha au dhummah
2.Inakapokuwa na sakinah na nyuma yake kuna herufi yenye fataha au dhumah
3.Itakapokuwa na sakinah na nyuma yake kukawa na kasra na mbele yake kukawa na herufi za istiโ€™laa
4.Itakapokuwa ina sakina na nyuma yake kukawa na hamzatul-waswl yaani hamza ya kuungia.
5.Itakaposimamiwa kwa sakina halafu nyuma yake kukawa na sakina na nyuma ya hiyo sakina kukawa na fataha au dhumah.

Pia itakuwa nyepezi au nyembaba itakapokutana na hali zifuatazo;-
1.itakapokuwa na kasra
2.Itakapokuwa na sakina na nyuma yake kuna fataha
3.Itakaposimamiwa na sakina na kukawa nyuma yake kuna sakina iliyotanguliwa na kasra.
4.- 5 Inayoitwa ุงู„ุฑุงุก ุงู„ู…ู…ุงู„ุฉ (ar-raa al-mumaalah) ambayo inasomwa kwa vokali ya โ€˜eโ€™ badala ya kasrah. Hii ni kutokana na riwaayah ya Hafsw โ€˜an Aaswim. Nayo ni katika neno la pekee katika Qur-aan, na huwa ni ya tarqiyq inapatikana katika surat hud aya ya 41 (11:41)


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 1837

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰3 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰4 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq

Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.

Soma Zaidi...
Faida za kujuwa Quran tajwid

Hapa nitakufindisha faida za kusoma quran kwa Tajwid.

Soma Zaidi...
Kwa nini quran ilishuka kidogo kidogo?

Kuna sababu nyingi za kuonyesha umuhimu wa Quran kushuka kwa mfumo wa kidogo kidogo

Soma Zaidi...
WAQFU WAL-IBTIDAAI

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka Surat al Kafirun

Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.

Soma Zaidi...
Hoja juu ya kukubalika hadithi

Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...