(iii)Dai la Kujidhania Kupata Wahy (Self Revelation)
Bwana E. Birmngham katika kitabu chake anadai kuwa, kwa sababu Muhammad (s.a.w) alikuwa mkweli na mwadilifu alichukia sana moyoni mwake kwa jinsi uovu na ufisadi ulivyoshamiri katika jamii yake. Kutokana na mwangaza aliokuwa nao yeye mwenyewe binafsi akaona kuwa ipo haja ya kuijenga upya jamii hiyo. Huenda pia alisikia juu ya kitabu cha Wayahudi na Wakristo lakini hakupendezwa na mafundisho ya Utatu Mtakatifu (Trinity). Na yawezekana alisikia kuwa atakuja nabii kutoka katika eneo hilo. Mambo hayo yakawa yanazunguka ndani kabisa ya nafsi yake, hadi kufikia kuamini kuwa yeye ni mtume na ndipo akaanza kupata fikra za kimazezeta kuwa Malaika wanamsemesha.
Udhaifu:
Endapo kama chimbuko la Qur-an ni hisia za ndani za nafsi ya Muhammad (s.a.w) (subconsciousness), basi Qur-an itakuwa inatokana na elimu na mazingira yake. Lakini ukiiangalia Qur-an kwa makini utaona kuwa imetoa taarifa nyingi sana ambazo itakavyokuwa vyovyote haziwezi kuwa zimetoka katika nafsi ya Muhammad (s.a.w).
Kwa mfano Qur-an inaeleza matukio ya kihistoria au matukio yatakayotokea baadaye ambayo Muhammad(s.a .w) hakuyajua na wala hakuwa na namna ya kuyajua. Kwa mfano:
(1 )Sura ya 18 ya Qur-an, Al-Kahf iliteremka baada ya Muhammad (s.a.w) kuulizwa maswali matatu na makafiri wa Makka ili kumjaribu. Maswali hayo waliyauliza baada ya kushauriana na watu wa Kitabu (Mayahudi). Maswali hayo yalikuwa:
(i)Ni kipi kisa cha vijana wa pangoni?
(ii)Ni kipi kisa cha Al-Khidhr?
(iii)Unajua nini juu ya Dhul-qarnain?
Kwa kuwa maswali haya yalifungamana na historia ya Wakristo na Wayahudi, na habari zake hazikujulikana Hijaz, yalikusudiwa kumpima Mtume (s.a.w) kuwa kweli alikuwa Mtume wa Allah (s.w) aliyekuwa akipokea wahy kutoka kwake au ni mzushi tu.
Alipoulizwa maswali hayo Muhammad (s.a.w) alisema, "Nitakujibuni kesho" lakini hakusema, 'I nshaa-Allah'. Siku iliyofuata alikuwa bado hajapata wahy, hivyo walipokuja makafiri kusikiliza majibu, akawaambia waje siku iliyofuata. Walipokuja hakuwa na majibu. Hali ikaendelea hivyo kwa muda wa siku 15. Makafiri wakaanza kumkejeli na kumdhihaki. Muhammad (s.a.w) akahuzunika sana kwa kutopata wahy alioutazamia. Hatimaye Jibril (a.s) akamletea wahy akafahamishwa majibu ya maswali yote. Kule kuchelewa kuja kwa wahy kulikuwa ni fundisho kwake:
Wala usiseme kamwe kwa lolote lile kuwa: "Nitalifanya kesho." Isipokuwa (uongeze) Ishaa-Allah. Na umkumbuke Mola wako unaposahau, na useme "Asaa Mola wangu ataniongoza njia iliyo karibu zaidi na uongofu kuliko hii" (18:23-2 4)
Ingawa kuchelewa kwa kuja wahyi kulimsononesha sana Muhammad (s.a.w) ilikuwa ni ushahidi kuwa Qur-an haikutungwa na yeye. Laiti angelikuwa mtunzi wa Qur-an angeliyatoa majibu yale kesho yake ili kuepuka fedheha iliyompata.
Kuhusiana na hili la fikra za kimazezeta jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Muhammad (s.a.w) aliulizwa maswali kuhusiana na matukio maalum,. Ni vigumu sana kuona jinsi ambavyo fikra za kimazezeta ya kidini zingeweza kumsaidia kujibu kwa usahihi maswali aliyoulizwa. Majibu ambayo yaliwatosheleza na kuwanyamazisha makafiri.
Na miongoni mwa mambo yanayojitokeza katika kisa hiki ni namna ulivyowasilishwa muda wa vijana waliokaa pangoni. Qur-an inasema: Na walikaa katika pango yao miaka mia tatu, na ongeza tisa. (18:25)
Kwa nini aya haikusema moja kwa moja "miaka mia tatu na tisa" na badala yake ikasema "mia tatu na ongeza tisa?" Hii ni kwasababu vijana hao walikaa miaka 300 kwa kufuata kalenda ya jua (solar calendar) na ni miaka 309 kwa kufuata kalenda ya kuandama mwezi (lunar calender). Sababu yake ni kuwa mwaka wa kuandama kwa miezi ni mfupi kwa siku 11 ukilinganishwa na ule wa jua. Hivyo 11 X 300/365 = 9. Yaani siku 11 mara 300 kugawanywa kwa 365 ni miaka 9. Hivyo basi madai kuwa mahesabu hayo sahihi yanatokana na kujidhania au mauzauza yaliyompanda Muhammad (s.a.w) hayana nguvu. Mfano mwingine tunaukuta katika sura ya 89 ya Qur-an ambayo ina aya inayoutaja mji wa kale sana wa Iram:
Je! Hukuona jinsi Mola wako alivyowafanya Adi, wa (mji wa) Iram, wenye majumba marefu marefu ambayo hawakuumbwa mfano wao katika miji (mingine) ." (89:6-8)
Jina la mji huu lilikuwa halijulikani vizuri hata wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w). Kwa sababu hiyo kulikuwa na utatanishi mkubwa juu ya ni ipi Jiografia ya mji huo.
Hata hivyo utafiti uliochapishwa katika jarida la chama cha Jiografia huko Marekani liitwalo The National Geographic toleo la December 1978 umeonesha kuwa Iram ni jina la mji. Mwaka 1975 Dk. Paolo Mathiae wa chuo Kikuu cha Roma aligundua huko Syria maktaba ya kale sana iliyokuwa na vigae 15,000 vyenye maandishi. Miongoni mwa maelezo yaliyokuwamo katika vigae hivyo ilikuwa ni taarifa kuwa watu wa mji wa Ebla walikuwa wakifanya biashara na watu wa mji wa Iram.
Ni vigumu sana kuona ni kwa vipi fikra za kizezeta zingeweza kumwongoza Muhammad (s.a.w) kutoa taarifa sahihi juu ya majumba yaliyoharibiwa miaka 3,000 kabla yeye hajazaliwa! Isitoshe Qur-an imetamka katika sehemu kadhaa kuwa Muhammad na watu wake hawakuvijua baadhi ya visa vilivyotajwa katika Qur-an:
Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla ya hii (Qur-an kuteremshwa). Hakika mwisho mwema ni wa wamchao Mwenyezi Mungu (11:49)
Yafaa kuzingatia hapa kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza na kusema, "Ewe Muhammad, hayo uyasemayo si kweli. Mimi ni Mwarabu kama wewe na nilizijua habari hizi kabla ya huu wahy wako. Si hivyo tu, bali pia kama Muhammad (s.a.w) angekuwa ndiye mtunzi wa Qur-an asingethubutu kuitamka aya hii, au kama angeitamka basi angekuwa amejitia katika patapotea ya hatari kabisa kwa sababu zifuatazo:
Kwanza, hata kama tukisema mathalan kuwa Muhammad (s.a.w) kwa hakika alizijua habari hizo kabla lakini hapa anasingizia tu, basi hapana shaka yeye hatakuwa mtu pekee anayezijua. Hivyo asingeweza kusema kwa ujasiri kiasi hiki juu ya kutokujua kwa wengine. Atakuwa na uhakika gani kuwa watu wote wengine hawazijui?
Pili, hata kama ni kweli kuwa watu wengine hawakujua habari hizo, maadui na wapinzani wake wangeweza kusingizia kuwa wao kwa hakika walikuwa wanazijua habari hizo hasa hasa ilivyokuwa kauli hiyo imetamkwa katika Qur-an baada ya kumaliza kukisimulia kisa chenyewe. Lakini pamoja na yote hayo hakuna mtu aliyeitumia fursa hiyo. Muhammad (s.a.w) angewezaje kujua kuwa hakuna mtu atakayeitumia fursa hiyo?
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 530
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitabu cha Afya
As-Sab nuzul
Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran. Soma Zaidi...
Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia
Soma Zaidi...
quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...
Kutokea Kweli Matukio yaliyotabiriwa katika Qur-an
Soma Zaidi...
QURAN: TAJWID, FADHIKA ZA KUSOMA QURAN, FADHILA ZA KUSIKILIZA QURAN, FAIDA ZA SURAT FATIHA, YASIN, BAQARA, TABARAK
Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat at Takaathur
Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi Soma Zaidi...
Nini maana ya Iqlab katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa Surat At-Takaathur
Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii surat At-Takaathur ilishuka Makka, na hizi ndio sababu za kushuka kwa sura hii Soma Zaidi...
Madai ya makafiri dhidi ya quran na hoja zao
Soma Zaidi...
Hukumu ya Ikhfau katika tajwid
Ikh-fau ni moja ya hukumu za nun sakina na tanwin kwenye hukumu za Quran tajwid Soma Zaidi...
Sababu nyengine zilopelekea kushushwa kwa suratul ikhlas
Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Quran
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...