picha

HUKUMU ZA MADD

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

HUKUMU ZA MADD

SURA YA KUMI
MADD-Madd-Twab'iy
MADD
Katika hukmu ya Tajwiyd ni urefushaji au uongezaji wa sauti, kwa maana kuivuta sauti ya herufi wakati inapokutana na moja ya herufi za madd kuifanya iwe ndefu.
Herufi za madd ni tatu:
ا • Alif saakinah iliyotanguliwa na fat-hah: قَالَ
ي • Yaa saakinah iliyotanguliwa na kasrah: قِيلَ
و • Waaw saakinah iliyotanguliwa na dhwammah: يَقُولُ

Madd imegawanyika sehemu mbili kuu:
الْمَدُّ الطَبِيعي • Al-Maddutw-Twabiy’iy pia huitwa: الْمدّ الأصْلي - Al-Maddul-Aswliy
الْمَدّ الْفَرْعي • - Al-Maddul-Far-’iy

1.Maddu-twabiy’y
Hii ni madd ya asili ambayo madd zote zimepatikana kutoka hapa. Maddd hii ni ya haraka 2 na haijuzu kuzipunguza wala kuzizidisha na ni makosa kufanya vinginevyo. Madd hii itavutwa katika hali zote ima katika hali ya kuunganisha maneno au katika hali ya kusimama. Ili itokee madd hii haihitaji sababu zingine ila ni asili ya neno tu ni lazima liwe na madd hiyo.
MADD

Halikadhalika madd hii kuna maeneo saba ambayo haipatikani wakati wa kuunga maneno ila itapatikana tu pale msomaji anaposimama. Na sehemu hizi zipo saba tu na zinapatikana kwa kuwepo alif na hii huitwa jina la الْفات السبع (Alifaatus-Sab-‘iy - Alif Saba).
MADD

(maddutw-twabiy’iy) nyinginezo ni:
مَدُّ الصِّلَّةِ الصُّغْرى . 1 - Maddusw-Swillatis-Sughraa
2 مَدُّ الْعِوَضِ . - Maddul-‘Iwadhw
مَدُّ الْبَدَل . 3 – Maddul-Badl
مَدُّ التَّمْكِين . 4 – Maddut-Tamkiyn
ألِفَات حَيُّ طَهْر . 5 – Alifaatu Hayyun Twahr

. 1 Maddusw-Swillatis-Sughraa:
Swillah ni kuunganisha herufi ya ه (haa) ya kiwakilishi1 na herufi ya madd yenye kunasibiyana na i’raab yake (dhwammah au kasrah) kitakapokuwa hicho kiwakilishi cha ه ni chenye i’raab na kipo baina ya herufi mbili zenye i’raab. Swillah hii imegawanyika sehemu mbili mojawapo ni hii ya assughraa (ndogo) na ya pili yake ni ya al-kubraa (kubwa) itakayokuja maelezo yake katika Maddul-Far-’iy.
Shart zake:
i) Kuweko na i’raab (sio sukuwn au herufi ya madd) kabla ya ه (haa)
ii) Kuweko na i’raab ifuatie katika neno la pili.
iii) Haifuatwi na hamzah.
MADD


Hukumu hii haizingatiwi katika maeneo mawili kwenye qurani. Aya hizi moja wapo huvutwa (Al-Furqaan (25: 69) ) ijapokuwa haina sifa za kuvutwa na nyingine haivutwi (Az-Zumar (39 : 7)) ijapokuwa ina sifa za kuvutwa. Na hii ni kutokana kuwa hivyo ndivyo inavyosomwa. Maeneo hayo ni haya;-
MADD

(Az-Zumar (39 : 7) Al-Furqaan (25: 69)

. 2 Maddul-Badal
Kanuni ya badal: ni kuja kwa hamzah mbili zenye kufuatana moja baada ya nyengine, ya kwanza ikawa na i’raab na ya pili ikawa saakin katika neno moja, hivyo hubadilishwa hamzah ya pili saakinah na kuwa herufi ya madd yenye kuwiana na i’raab ya hamzah ya kwanza. Hukmu yake ni kuvutwa harakah mbili.
MADD


Maddul-‘Iwadhw
Ni madd inayotokea wakati wa kusimama msomaji katika neno lenye fathataan (tanwiyn fat-hah). Hukmu yake ni huvutwa kwa harakah mbili. Kusimama kwenye ة (taa marbuwtwah ya kike iliyofungwa) kunapelekea kutokuwepo hukmu hii ya مَدُّ الْعِوَض (maddul-‘iwadhw) kwani wakati huo huondoka tanwiyn na kusimamiwa kwa ه (haa) saakinah.

4.Maddut-Tamkiyn
Ni madd inayotokea wakati ي mbili zimekutana, ya kwanza ina shaddah na kasrah na ya pili ina sukuwn. Imeitwa مَدُّ التَّمْكِين kwa sababu inatamkwa ikiwa imethibitika kwa sababu ya shaddah. ي ya pili ambayo ina sukuwn inavutwa kwa harakah mbili.
MADD


5 - Alifaatu-Hayyin-Twahur
Ni مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy) inayotokana katika kutamkwa baadhi ya الحروف المتقاطعة (Al-Huruwf Al-Mutaqatw-twa’ah)1 zinazoanzia baadhi ya
Suwrah, kwa vile herufi hizo zinatamkwa kama herufi za hijaaiyah طا حا
ها را . Nazo zimeundwa katika ibara ya حيّ طهر (hayyun twahur) kwa jina
jingine huitwa ألِفَاتُ حَيٍّ طَهُ ر (Alifaatu hayyin twahur).
MADD


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 1672

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Fadhila za kusoma surat al Kahaf siku ya Ijumaa

Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili

Soma Zaidi...
Fadhila za kusoma surat al Baqarah

Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii.

Soma Zaidi...
ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN

ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa Surat At-Takaathur

Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii surat At-Takaathur ilishuka Makka, na hizi ndio sababu za kushuka kwa sura hii

Soma Zaidi...
Ni ipi aya ya mwisho kushuka katika Quran?

Maulamaa katika elimu ya Quran wametofautiana juu ya aya ya mwisho kushuka. Hata hivyo hapa nitakutajia ambayo imependekezwa zaidi

Soma Zaidi...
quran na sayansi

YALIYOMONENO LA AWALI1.

Soma Zaidi...