Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi.
Maana na majina ya Quran
Maana ya Wahyi.
Ni ufunuo kutoka kwa Allah (s.w) kwenda kwa wanaadamu (mitume) kupitia Malaika wake Jibril (a.s). Wahyi umegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni Qurani na Hadithi. Wahyi umekuwa ukimjia Mtume na mitume wengine walotangulia kupitia malaika jibril. Lakini zipo njia nyingine ambazo wahyi unaweza kuwajia wanadamu. Njia hizo ni;-
1.Il-hamu
2.Kusemeshwa na Allah (s.w) nyuma ya pazia.
3.Kupitia malaika.
4.Ndoto za kweli.
4.Maandishi.
Qur’an ni maneno ya Allah (s.w) yaliyoteremshwa kwa Mtume (s.a.w) kwa njia ya wahyi kupitia Malaika Jibril (a.s) ili kuwa mwongozo kamili wa maisha ya wanaadamu. Qurani imekuwa ikitambulika kwa majina mengi sana yakiwemo;-
Al-Qur’an – Chenye kuunganishwa pamoja au chenye kusomwa.
Kalamullah – Maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Al-Mas-haf – Mkusanyiko wa kurasa nyingi (Kitabu kikubwa).
Al-Kitabu – Kitabu Pekee (The Unique Book) Kimuundo, Kimaudhui,
Kiusahihi, n.k.
Al-Furqaan – Kipambanuzi baina ya haki na batili.
Adh-Dhikru – Mawaidha au Ukumbusho.
At-Tanziil – Kiteremsho (Mshuko), Wahyi kutoka kwa aliye juu.
Al-Hukmu – Kitabu pekee kinachostahiki kumhukumu binaadamu.
Al-Hikma – Kitabu pekee chenye hikima isiyo na kikomo
(Kitabu cha Hikima).
Ash-Shifau – Ponyo au dawa pekee ya kuponya nafsi, nyoyo, uasi, ukafiri, n.k.
Ar-Rahma – Rehema kwa wanaadamu.
Al-Khayr – Kheri pekee, Qur’an ndio chanzo cha kheri zote.
Ar-Ruuhu – Roho ya maisha, asiyeishi kwa mujibu wa Qur’an ni maiti.
Al-Bayaana – Chenye kuweka wazi, kubainisha kila kitu kwa uwazi, n.k.
An-Nuur – Nuru peke ya kumuangazia binaadamu katika njia sahihi ya
maisha.
Al-Burhan – Hoja zilizo wazi, zenye kueleweka kwa kila mwenye akili.
Al-Haqq – Kitabu cha Haki, kinachotoka kwa Mola wa Haki kwa ajili ya
Kusimamia haki.
Ahsanul-Hadith – Simulizi, maelezo, hadith nzuri kuliko zote.
Al-Hudaa – Mwongozo pekee sahihi wa maisha ya mwanaadamu.
Qur’an ni Kitabu chenye aya 6,236, zilizo katika sura 114 na kimegawanywa katika Juzuu (mafungu) 30. Pia inatupasa tujuwe kuwa qurani kabla ya kumfikia mtume ilipitia hatuwa kuu mbili a,bazo ni;-
Qur’an imeshuka katika hatua kuu mbili;
1.Imeshuka jumla kutoka Lawhim-Mahfuudh (Ubao uliohifadhiwa katika Arshi) hadi Mbingu ya Dunia.
2.Kushuka kidogo kidogo duniani kuja kwa Mtume (s.a.w) kupitia Malaika Jibril (a.s) kwa muda wa miaka 23.
Rejea Qur’an (85:21-22), (81:19-20)
Mtume (s.a.w) alianza kushukiwa na wahyi wa kwanza wa Qur’an mwaka 610 A.D akiwa na umri wa miaka 40 katika pango la ‘Jabal Hiraa’. Qur’an ilianza kushushwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Usiku wenye cheo wa “Lailatul – Qadri”. Rejea Qur’an (97:1-5) na (2:185). Ilianza kushuka kwa aya 5 za mwanzo katika suratu Alaq (96:1-5).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1138
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Kitabu cha Afya
Nguzo 6 za iman ya dini ya kiislamu kwa mafundisho ya quran na sunnah
Nguzo za Imani. Soma Zaidi...
Kuamini qadar na qudra katika uislamu
Kuamini Qadar ya Allah (s. Soma Zaidi...
Ni nini maana ya ndoa?
Soma Zaidi...
quran na sayansi
Soma Zaidi...
NASAHA ZANGU NNE KWAKO KUHUSU QURAN, MAUTI, DUA NA MENGINE
Soma Zaidi...
Sababu za kushuka sura kwenye quran na fadhila za sura mbalimbali kwenye quran
Soma Zaidi...
Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?
Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu? Soma Zaidi...
Namna ya kutufu, na masharti ya mwenye kutufu
3. Soma Zaidi...
nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...
Hukumu ya zakat Al-Fitir na namna ya kuitoa zaka ya fitir
Soma Zaidi...