Kusimamisha Swala.
Kusimamisha Swala.
Maana ya Kusimamisha Swala Kusimamisha swala ni tofauti na kuswali. Kuswali ni kufanya vitendo vya swala kama vile kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, n.k.
Kusimamisha swala ni kuitekeleza swala kwa kuchunga na kutekeleza kwa ukamilifu yafuatayo:
(i) Sharti zote za swala.
(ii) Nguzo zote za swala.
(iii) Kuwa na khushui (unyenyekevu) wakati wote wa kutekeleza sharti na nguzo za swala.
Mtu akiswali bila ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu mambo haya matatu, ataonekana kuwa kaswali, lakini atakuwa hajasimamisha swala na atastahiki kuadhibiwa vikali na Mola wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: ยBasi adhabu kali itawathibitikia wanaoswali, ambao wanapuuza swala zao (kwa kutozisimamisha), ambao hufanya riaย (107:4-6).
Kupuuza swala ni pamoja na kutotekeleza ipasavyo sharti za swala, nguzo za swala, na kutokuwa na unyenyekevu wakati wa kutekeleza sharti na nguzo za swala. Hivyo, swala inayokubalika mbele ya Allah (s.w) ni ile iliyosimamishwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: ยHakika wamefuzu waumini ambao katika swala zao ni wanyenyekevuย. (23:1-2) ยNa ambao swala zao wanazihifadhiย. (23:9) Kuhifadhi swala ni kutekeleza kwa ukamilifu sharti na nguzo zote za swala.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi
Soma Zaidi...Aina za Swala za Sunnah.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุนูููู ุดูุฏููุงุฏู ุจููู ุฃูููุณู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุนููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ุฅููู ุงูููููู ููุชูุจู ุงููุฅูุญ...
Soma Zaidi...Kuchungaย au kutekelezaย ahadiย ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli.
Soma Zaidi...Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha
Soma Zaidi...Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali.
Soma Zaidi...