image

Watu hawa huruhusiwi kuwaoa katika uislamu

Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.

Umaharimu

Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba kama ilivyobainishwa katika Qur-an na Sunnah. Wanaume wa Kiislamu wameharamishiwa kuwaoa wanawake wanaobainishwa katika aya zifuatazo:

 

Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu; isipokuwa yale yaliyokwishapita. Bila shaka jambo hili ni uovu na chukizo na ni njia mbaya (kabisa). Mmeharamishiwa (kuoa) mama zenu, watoto wenu, dada zenu, shangazi zenu, ndugu za mama zenu, watoto wa ndugu zenu, watoto wa dada zenu, na mama zenu waliowanyonyesheni, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, walio zaliwa na wake zenu mliowaingilia. Lakini kama nyinyi hamjawaingilia basi si vibaya kwenu (kuwaoa). Na mmeharamishiwa wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na (mmeharamishiwa) kuwaoa madada wawili wakati mmoja, isipokuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kurehemu na Mwenye kusamehe. (4:22-23)

 

"Na pia mmeharamishiwa wanawake wenye (waume zao) isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ndiyo Sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) minghairiya hawa..." (4:-24)

 


Aya hizi zinabainisha wanawake walioharamishwa kuwaoa kuwa ni hawa wafuatao:
1.Mwanamke aliyepata kuolewa na baba yako, (babu yako, baba wa baba yako - wa kuumeni na kikeni).
2.Mama aliyekuzaa (babu aliyezaa waliokuzaa, mama wa bibi aliyezaa aliokuzaa...).
3.Binti yako uliyemzaa (au binti aliyezaliwa na uliyemzaa...). Pia binti wa kunyonya na mwanao (na kikazi chake...).
4.Dada yako khalisa au wa kwa baba au wa kwa mama.
5.Shangazi yako- dada wa baba yako,(na dada wa babu yako...).
6.Mama mdogo; ndugu wa mama yako (au ndugu wa bibi yako...).
7.Binti wa ndugu yako mwanamume, khalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa naye).
8.Binti wa dada yako khalisa au wa kwa baba au kwa mama


9.Mama wa kukunyonyesha (na mama zake wa kumzaa au wa kumnyonyesha).
1O.Dada yako wa kunyonya naye (aliyenyonyeshwa na aliyekunyonyesha).


11 .Mama yake mkeo wa kumzaa au wa kumnyonyesha (na bibi yake pia wa kumzaa mama yake au wa kumnyonyesha Ama ndugu yake mama yake mkeo yaani mama mdogo wake au shangazi yake wa kuzaliwa au kunyonya; unaweza kumuoa akifa mkeo au utakapomuacha na eda ikaisha.
12.Binti wa mkeo uliyemuingilia (na mjukuu wake...).


13.Mke aliyeolewa na mwanao wa kumzaa au wa kunyonyeshwa na mkeo (na kizazi chake); si mke wa mtoto wa kupanga au mtoto wa kulea.


14.Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja. Akifa mke au ukimuacha na eda ikaisha unaweza kumuoa dada yake, au shangazi yake, au mama yake mdogo.


15.Mke wa mtu, bado mwenyewe hajafa wala hajamuacha ni Haram kumuoa. Wanawake hao wameharamishwa kuolewa na wanaume wanaofanana na hawa kwa upande wa kiumeni.


 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1820


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

NAMNA YA KUSWALI
13. Soma Zaidi...

Ni watu gani wanaopewa Zaka
Soma Zaidi...

Ni wakina nani ni lazima kwao kufunga ramadhani?
Soma Zaidi...

Ujuwe utaratibu mzima wa funga na kutekeleza ibada ya Swaumu
Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi.
Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla. Soma Zaidi...

Misingi na Maadili Katika Uislamu
5. Soma Zaidi...

Mambo gani ni Haramu kwa mwenye janaba?
Hadathi ya kati na kati (Janaba). Soma Zaidi...

Nguzo za swaumu (kufinga)
Hapa utajifunza nguzo kuu za swaumu. Kama hazitatimia nguzo hizi basi swaumu itakuwa ni batili. Soma Zaidi...

Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...

Kumuandaa Maiti kabla ya kufa ama kukata roho
Soma Zaidi...

Usawa katika uchumi wa kiislamu
5. Soma Zaidi...