kwa nini riba ni haramu?
Uharamu wa Riba katika Uislamu
Kwanza, Uislamu umeharamisha riba kwa sababu ni dhulma (unyonyaji).Ukichukua mkopo wa riba uliochukuliwa kwa madhumuni ya kukidhi haja ya matumizi ya lazima ya nyumbani, utozaji wa riba unakiuka lengo la Allah la kuumba (kuleta) mali kwa wanadamu. Utaratibu aliouweka Allah ni kwamba kwa kuwa mali ameileta kwa wanaadamu wote:
“Yeye (Allah) Ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi...” (2:29).
Ni lazima matajiri (wenye mali) wawapatie wanyonge na wenye dhiki mahitaji yao muhimu ya maisha.
Pili, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu inahamisha mali kutoka kwa maskini au wanyonge na kuipeleka kwa tajiri ambayo huzidi kuondoa usawa katika mgawanyo wa mali. Hii ni kinyume na mahitaji ya jamii. Uislamu unataka kila mtu apate mahitaji muhimu ya maisha. Hivyo wale walio na ziada ya mahitaji muhimu ya maisha wanatakiwa wawape wasionacho kabisa au wale waliopungukiwa kwa upendo na udugu. Riba inakanusha kabisa msimamo huu.
Tatu, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu hufanya kundi la watu katika jamii liishi kivivu bila ya kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji, likitegemea kuishi kwa riba kutokana na mali zao walizozikusanya katika mabenki, bima, na vyombo vingine vya riba. Jamii inakosa mchango wa watu hawa katika uzalishaji na si hivyo tu, bali watu hawa wanakuwa mzigo na bughudha katika jamii. Ufasiki (uharibifu) wa aina zote katika ardhi hufanywa na kundi hili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 ai web app 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Mwenendo wa mwenye kunuia hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Baada ya kumzika maiti nini kifanyike kumsaidia marehemu
Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo.
Soma Zaidi...Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.
Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi.
Soma Zaidi...Masharti ya swala
Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...Kusimamisha Swala na kuamrisha mema
Swala iliyosimamishwa vilivyo ndiyo nyenzo kuu ya kumtakasa Muislamu na kumpa sifa zinazomuwezesha kustahiki kufanya kazi takatifu ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
Soma Zaidi...