image

Hadhi na Haki za Mwanamke Ulaya chini ya kanisa hapo zamani

Hadhi na Haki za Mwanamke Ulaya chini ya kanisa hapo zamani

(c) Ulaya Chini ya Kanisa



Ukristo ulipoingia Ulaya uliisaidia jamii kuondoa mila chafu na kukomesha mwenendo mchafu wa wanawake kuuza miili na utu wao kwa wanaume. Pamoja na jitihada hizi bado, mafundisho ya Ukristo yalizidi kumyanyasa mwanamke na kumuona yeye kuwa ndio chanzo cha matatizo yote katika jamii. Hapa tutajaribu kunukuu maandiko machache ya Watakatifu na viongozi wa Kanisa kuonesha ukristo ulivyomnyanyasa na kumnyanyapaa mwanamke.


Mawazo ya Paulo, ambaye ameandika vitabu 14 kali ya vitabu 27 vyaAgano Jipya, yanaathari kubwa kalika historia ya Ukiisto. Paulo anawahesabu wanawake kuwa ni waovu kwa hi& anawapiga marufuku kuftindisha:



Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna, simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. (Timotheo 2:11-14).
Zaidi ya hivyo, Paulo anasema wanaume ni mfano wa utukufu lakini wanawake ni utukufu wa mwanamume:



Lakini nataka mjueya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni wanamume, na kichwa cha Kiristo ni Mungu... Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano wa utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume... Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani. (Wakorintho 11:3, 7, 10).



Paulo ambaye hakupata kuoa katika maisha yake anarudia mitholojia ya nyoka kusisitiza jinsi mwanamke anavyodanganywa:
"Lakini nachelea, kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, as/e akawaharibu fikra zenu mkaacha unyoofu na usafi kwa Kristo ". (Wakorintho 11:3).
Pamoja na maandiko haya ya Paulo kuna maandishi mengi mengineyo ya viongozi wa kanisa ambayo yamewaelezea wanawake kama viumbe viovu kabisa. Akitoa muhtasari wa msimamo wa viongozi wa kanisa, mwanahistoria mashuhuri, Bwana Leakey ameandika hivi:



This pious incentive, which formed so conspicuous and so grotisque a portion of the writing ofthefathers... Woman was represented as the door of hell as the mother of all human ills. She should be athamedat the veiy thought that she is a woman. She should live and continue in penance on account of the curse she has bmught woon the world She should be ashamed of her dress for it is a memorial of her fall she should be especially ashamed of her beau!y for it is the most potent instrument of the devil.



Tafsiri:
Kilichoko hiki kitakatfu kilichozusha maandishi ya kutisha ya Mapadre... mwanamke alitajwa kama mlango wa Jahannam na mama wa maovu yote ya binadamu. Fikra tu ya kuwa yu mwanamke yampasa aone aibu. Aishi na adumu katika matubio kwa sababu ya laana aliyoileta duniani. Hana budi kulionea haya vazi lake kwani ni kumbukumbu ya kuanguka kwake (dhambini), na hasa hasa auonee aibu urembo wake kwani hiyo ni silaha kubwa ya shetani.



Tertullian Quintus Septimius Florens (160 A.D - 220 A.D) naye ameandika juu ya Mwanamke. Miongoni mwa maandiko yake ni haya yafuatayo:
You are the devils, getway, you are the ... of the forbidden tree, you are the first deserters of the divine law. You are she who persuaded him whom the devil was not valiant enough to attack. You destroyed so easily God's image, man. On account for your deserving death even as the son of God had to die.



Tafsiri:
Wewe (mwanamke) ni mlango wa shetani, wewe ndiye... wa mti uliokatazwa, wewe ndiye wa kwanza kuitelekeza sheria ya Mungu. Wewe ndiye (yule mwanamke) aliyemshawishi yule (mwanamume) amabye shetani hakuweza kumshambulia. Wewe ulimharibu kirahisi sana yule ambaye ni mfano wa Mungu, (yaani) mwanamume. Kwa sababu ya dhambi zako mwana wa Mungu (yaani Yesu) ilibidi afe (msalabani).


Maandiko haya yanaonesha Ukristo unavyomnyanyasa mwanake.


Ni katika imani ya Kikristo kuwa mwanamke ni chanzo cha dhambi, kutokana na madai yao kwamba ni Hawa aliyemhadaa mumewe Adam wakala tunda katika mti waliokatazwa huko Peponi kabla ya kuletwa kwao hapa duniani. Wakristo wanaamini kuwa kama Hawa asingalimhadaa Adam wakala tunda pasingalikuwa na maisha haya machungu ya hapa duniani bali mwanaadamu angali bakia na uzima wa milele huko peponi. Kutokana na imani ya Wakristo, dhambi hii ya asili aliyoisababisha mwanamke wa kwanza, haikusamehewa kwa mwanaadamu mpaka alipokuja Yesu kumkomboa mwanaadamu kutokana na dhambi hii kwa kujitoa muhanga huko msalabani.



Pamoja na itikadi hii ya Dhambi ya Asili, itikadi nyingine ya Wakristo ni kwamba kitendo cha jimai ni kitendo kiovu na kichafu hata kama mume na mke wamefunga ndoa ya halali. Pia ni katika msingi huu kukaa bila kuoa au kuolewa, imedhaniwa na Wakristo Wakatoliki kuwa ni kitendo cha hali ya juu cha ucha-Mungu. Kwa mtazamo huu kuoa kumefanywa kuwa jambo ovu lisilo budi. Itikadi hii iliifanya jamii ya Kikristo ione kuwa ndoa ni mzigo mkubwa kwa mwanamume na mwanamke.
Tumejifunza katika sheria ya familia ya huko Ulaya chini ya kanisa kuwa:



(1)mwanamke alinyimwa haki za kiuchumi na alifanywa amtegemee mwanamume moja kwa moja. Alipewa sehemu ndogo tu ya urithi, alikuwa na haki finyu sana za kuchuma mali, hakuwa na mamlaka juu ya mali yake aliyoichuma kwani hii ilikuwa katika mamlaka ya mumewe ambaye alikuwa na haki zote juu yake.



(2)Talaka iliharamishwa kabisa katika sheria hii. Mume na mke walilazimika kuishi pamoja mpaka wafe hata kama hawakuelewana. Katika kiwango kikubwa cha kutoelewana, mke na mume wanaruhusiwa kutengana lakini hapana ruhusa kuoa au kuolewa tena. Hatua hii iliwafanya wawili hawa kuwa watawa au kutumbukia katika ufuska.



(3)Ilionekana ni jambo Ia kuchukiza au dhambi kwa mtu kuoa au kuolewa tena, baada ya mke au mume kufariki. Ndoa baada ya kufiwa na mume au mke ilihesabiwa kama "uzinifu wa ama yake - "Civilized Adultery'.



Mtu akizingatia kwa makini mafundisho ya Ukristo juu ya mwanamke na sheria ya ndoa ya Kikristo, anaweza kuelewa kwa nini wanawake katika nchi za Kikristo huko Ulaya na Marekani walikuja yakataa mafundisho haya na kupigania haki ya kuwa sawa na wanaume. Kosa ambalo watu wengi hulifanya ni kudhani kuwa maadam Ukristo unamdhalilisha mwanamke, na Uislamu vile vile unamdhalilisha mwanamke. Na baadhi ya Waislamu ambao hawajafanya juhudi za kujifunza Uislamu na Ukristo wamejikuta wanasaidia kukuza dhana hii.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 417


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Jinsi uislamu ulivyokomesha biashara ya utumwa wakati na baada ya mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...

Namna ya kulipa swaumu ya ramadhani na ni nani anatakiwa alipe
Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za Mwanamke Ulaya chini ya kanisa hapo zamani
Soma Zaidi...

Wenye ruhusa za kutofunga ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake. Soma Zaidi...

Namna ya kuswali
2. Soma Zaidi...

Maana ya Ndoa na Faida zake katika jamii
4. Soma Zaidi...

Mambo yanayoharibu Udhu (yanayobatilisha udhu)
Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu. Soma Zaidi...

lengo la kuswali za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Fadhila za usiku waalylat al qadir
Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000. Soma Zaidi...

Maana na taratibu za kiuchumi katika uislamu
Soma Zaidi...