image

Namna ya Safari ya Hija inavyoanza

Namna ya Safari ya Hija inavyoanza

Safari ya Hija



Mtu aliyeisafia nia yake kwa ajili ya Hija na kwa ajili tu ya kutaraji Radhi za Mola wake, hupata zoezi kubwa kutokana na safari ya Hija la kumfanya awe tayari kujitoa muhanga kwa mali yake, nafsi yake na wapenzi wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w).



Tujuavyo, gharama ya safari ya Hija, ikiwa ni pamoja na usafiri, matumizi ya chakula, malazi, mnyama wa kuchinja, na kadhalika ni kubwa sana. Kwa mfano mwaka 1420/ 1999 gharama za Hija kwa Tanzania kwa wastani ilikuwa Shs. 700, 000/ -. Kwa tajiri kiasi hiki cha fedha kitaonekana si kikubwa sana, lakini ukizingatia kuwa hatarajii kupata malipo yoyote ya kidunia kutokana na fedha hiyo ila Radhi ya Mwenyezi Mungu (s.w) bado hali ya kujitoa muhanga inapatikana. Kwa mtu wa kawaida ambaye amepata gharama ya safari ya Hija kwa kulimbikiza kidogo kidogo kwa umri wake wote wa uchumi Tsh. 700,000/ - ni kiasi kikubwa sana kwake ambacho humpa zoezi kubwa sana la kuwa tayari kutoa mali yake wakati wowote na kiasi chochote kwa ajili ya kuihuisha na kuisimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w).



Mtu anapoaga kwenda Hija anakuwa tayari kwa moyo mkunjufu kuwaacha ahali zake, jamaa zake, rafiki zake na wapenzi wake wote ili akaitikie wito wa Mwenyezi Mungu (s.w). Kitendo hicho cha Haji kuwa tayari kuachana na wapenzi wake, kwa ajili ya safari ya Hija, humpa zoezi kubwa la kuwa tayari kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuliko chochote kingine. Hili ni zoezi muhimu sana kwa Muislamu kwani mtu hawezi kufuzu mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) mpaka kwanza aweze kumpenda Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake kuliko anavyoipenda nafsi yake na yoyote yule aliyempenzi kwake na kuliko anavyokipenda chochote kile chenye thamani kwake. Hebu tuzingatie usia wa Mwenyezi Mungu (s.w) ufuata



Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu (wanapenda) ukafiri kuliko Uislamu. Na katika nyinyi atakayewafanya hao kuwa ndio vipenzi vyake, basi hao ndio madhalimu (wa nafsi zao). Sema: Kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na mali mlizochuma na biashara mnazoogopa kuharibikiwa, na majumba mnayoyapenda, (ikiwa vitu hivi) ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni mpaka Mw enyezi Mungu alete amri yake; na Mw enyezi Mungu hawaongozi watu maasi. (9:23-24)



Kwa wastani safari ya Hija ni ngumu sana kwa watu wa kawaida (wasio wakuu wa Dola wanaopata mapokezi ya serikali ya Kifalme). Ugumu wa safari ya Hija unapatikana katika safari yenyewe, mabadiliko ya hali ya hewa, mkusanyiko wa watu wengi sana (milioni moja na zaidi) kwa wakati mmoja katika sehemu ndogo takatifu, msongamano katika kutekeleza baadhi ya nguzo za Hija kama vile kutufu, kusai na kutupa mawe katika minara mitatu. Kila mwaka watu hufa katika minara mitatu. Kila mwaka watu hufa katika sehemu hizi za msongamano. Ukimuuliza mtu yeyote wa kawaida aliyewahi kuhiji atakuhadithia zaidi juu ya uzito wa safari ya Hija. Ugumu huu wa safari ya Hija humpa Muislamu mazoezi ya kuitoa nafsi yake muhanga kwa kuwa yu tayari kukabiliana na magumu yote, hata ikibidi kufa kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa maana nyingine safari ya Hija inatupa funzo la kuwa tayari kupigania dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa nafsi zenu. Mtume (s.a.w) amelinganisha safari ya Hija na Jihad:



Aysha (r.a) am ehadithia: “Niliuliza: “Ee Mtum e w a Mw enyezi Mungu (s.w)! Kunajihadi kwa wanawake?” “Ndio” alijibu Mtume, ‘Kwao kuna jihadi isiyo ya kupigana’ - Haj na Umra’. (Ibn Majah).



Katika hadithi nyingine iliyosimuliwa pia na Aysha (r.a) Mtume (s.a.w) amesema:
“Jihad bora kw a (wanawake) ni Haj Mabruur (Haj yenye kukubaliw a)”.(Bukh ari)



Pia tunajifunza kutokana na Sunnah ya Mtume (s.a.w) kuwa Haji anayekufa katika vazi la Ihram, huzikwa na Ihram yake kama shahidi anavyozikwa na vazi lake la vita:
Ibn Abbas (r.a) ameeleza kuwa mtu mmoja akiwa katika vazi la Ihram (katika ha li ya Ihram) alianguka juu ya ngamia, akavunjika shingo na akafa. Mtume (s.a.w) alipofahamishwa habari hii aliamuru: “Muosheni kwa maji yaliyochanganywa na karafuuu maiti (leaves of the lot tree) na mumkafini kwa vipande viwili vya Ihram na msimfunike kichwa chake kw ani Mw enyezi Mungu (s.w) atamfufua siku ya Kiyam a akitamka Talbiya (akiitika Labbaya…)”.
Katika hadithi nyingine, Hijja na Jihad vimelinganishwa kama ifu atavyo:



Ames imulia Abuu Hurairah (r.a) kuwa mtume (s.a.w) aliulizwa: Ni kitendo gani kilichobora kuliko vyote? Akajibu: “Kumuamini Mw enyezi Mungu (s.w) na Mtume wake”. Akauliza tena: Ni amali gani inayofuatia kwa uzuri? Akasema: “Kufanya Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (s.w)”. Akaulizwa tena: Ni amali gani inayofuatia hii? Alijibu: “Kufanya Hija yenye kukubaliw a (Haj Mabruur)”. (Bukhari).



Hadithi zote hizi zinatupa fundisho kuwa safari ya Hija inatoa mafunzo ya Jihad kwa waumini.




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 803


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Sifa za Kuwa Mpole na Mnyenyekevu
22. Soma Zaidi...

Zijuwe funga za kafara na jinsi ya kuzigunga
Post hii itakufundisha kuhusu funga za kafara, zinavyotokea na na jinsi ya kuzifunga. Soma Zaidi...

lengo la kuswali za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa masikini, mafukara na wasio jiweza
Soma Zaidi...

Aina za tawafu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

namna ya kuswali swala ya vitani
Soma Zaidi...

MAFUNZO YA SWALA: NGUZO ZA SWALA, SHARTI ZA SWASL, FADHILA ZA SWALA, HUKUMU YA MWENYE KUACHA SWALA
Soma Zaidi...

NI ZIPI NGUZO NA SHARTI KUU ZA SWALA ILI IKUBALIWE
Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Soma Zaidi...

Swala za sunnah na faida zake
Soma Zaidi...

JIFUNZE IBADA YA FUNGA, NGUZO ZA FUNG, SUNNAH ZA FUNGA, FADHILA ZA FUNGA NA YANAYOHARIBU FUNGA.
Soma Zaidi...

Twahara
FIQH 1. Soma Zaidi...

Vipi funga yaani swaumu itapelekea uchamungu na kutekeleza lengo
Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu. Soma Zaidi...