Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Sunnah za Swala
Sunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Ama mwenye kuswali akiacha kipengele chochote katika vipengele vya sunnah, swala yake itakamilika iwapo atatekeleza vipengele vyote vya nguzo. Katika Hadith tumeona kuwa Mtume (s.a.w) katika swala yake pana vipengele vya ziada ya nguzo kama ifuatavyo:
1. Kuinua viganja vya mikono mkabala na mabega, usawa wa vigingi vya masikio wakati wa kuhirimia swala, kwenda kwenye rukuu, baada ya rukuu na baada ya kutoka kwenye Tahiyyatu ya kwanza.
2. Kusoma dua baada ya takbira ya kuhirimia.
3. Kuanza na afudhubillaah (kumlaani Shetani) kabla ya kuanza kusoma suratul-Fatiha.
4. Kuitikia Aaminhbaada ya kumaliza Suratul Fatiha.
5. Kusoma aya za Qur-an baada ya Suratul-Fatiha katika rakaa mbili za mwanzo. 6. Kuleta Tasbih, Tahmid na dua katika rukuu, itidali na sijda.
7. Kutoa takbira katika kubadilisha kitendo kimoja kuendea kingine isipokuwa tu kutoka kwenye rukuu kwenda kwenye itidali ndipo tunaposema: SamifAllahu liman hamidah - Rabbanaa lakal-hamdu.
8. Kukaa na kusoma Tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili, kwa swala zenye rakaa zaidi ya mbili.
9. Kusoma dua baada ya kumswalia Mtume na kabla ya kutoa Salaam.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la kusimamisha swala.
Soma Zaidi...