NINI MAANA YA SWALA (SALA AU KUSWALI), KILUGHA NA KISHERIA KATIKA UISLAMU

Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua.

NINI MAANA YA SWALA (SALA AU KUSWALI), KILUGHA NA KISHERIA KATIKA UISLAMU


Maana ya Swala
Maana ya Swala kilugha
(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua. Katika Qur-an tunaamrishwa kumswalia Mtume, yaani kumuombea dua Mtume (s.a.w) katika aya ifuatayo: Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (wanamtakia Rehema). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni au mtakieni Mtume) Rehema na muombeeni amani (33:56)

Vile vile katika Hadith, Mtume (s.a.w) anatuambia: Yule atakayealikwa kwenye karamu ya harusi aitikie wito huo, kama hataweza kuitika amswalie (amuombee dua) aliyemkaribisha. (Muslimu).

Maana ya swala Kisheria:
(b) Kisheria Katika sheria ya Kiislamu, swalaa ni maombi maalumu kwa Allah (s.w) yanayofanywa kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na Allah (s.w) na kufundishwa kwa matendo na Mtume wake. Katika maombi haya maalumu mwili mzima huhusika katika maombi haya kwa kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, kukaa na kuzingatia yale yote anayosema katika kuleta maombi haya.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Download App yetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 3124

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Nasaba ya mtume

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Ukasha bin Mihsan ni Sahaba aliyechangamkia Fursa

Katika somo hili utakwnda kujifunz anamna nambavyo Sahaba Ukasha alivyochangamkia fursa katika mambo ya heri

Soma Zaidi...