Ayyuub(a.
Ayyuub(a.s) ni katika Mitume wa Allah(s.w) waliotajwa katika Qur-an kwa umadhubuti wake katika imani juu ya Allah(s.w) na Subira.
Ayyuub(a.s) aliishi Kaskazini Mashariki ya Bara Arabu. Alikuwa tajiri sana mwenye mali nyingi, watoto wengi na watumishi wengi. Lakini hakutakabari bali alimuabudu Mola wake na kumshukuru ipasavyo
Nabii Ayyuub(a.s) alitahiniwa na Mola wake kama ifuatavyo:
(1) Mali yake, watoto wake na watumishi wake wote walipatwa na majanga wakatoweka. Akabakia yeye na mkewe ambaye naye alikuwa mcha-Mungu.
(2) Pamoja na kupotelewa na mali yake na watu wake wote, alishikwa na maradhi mabaya ya kuota vidonda mwili mzima kuanzia kichwani hadi miguuni. Alijaribu kutumia dawa zote alizoweza, lakini hakupata nafuu yoyote
Nabii Ayyuub(a.s) hakutetereka katika imani yake kutokana na majanga yaliyomfika bali alisubiri na kuwa karibu zaidi na Mola wake kuliko hata wakati alipokuwa katika hali yake ya mwanzo ya utajiri na afya nzuri. Na Allah(s.w) anamsifu mjawake, Ayyuub kama ifuatavyo:
“…. Bila shaka tulimkuta ni mwenye subira mja mwema; kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana.” (38:44)
Nabii Ayyuub(a.s) aliona kuwa aliyempa mali, watoto na wale watumishi aliokuwa nao ni Allah(s.w) kama amana. Hivyo, aliona hapakuwa na kosa lolote kwa Allah(s.w) kuchukua amana yake. Pia aliridhika na hali ya ugonjwa aliyokuwa nayo. Kwa ujumla Nabii Ayyuub (a.s) aliridhika na kusubiri juu ya matatizo yote yaliyomfika na kupata matunda ya subira kama Allah(s.w) anavyotubashiria:
Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi ya mambo haya); hofu na njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri.(2:155) Ambao uwapatapo msiba husema: “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea (atatupa jaza yake).(2:156)
Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema; na ndio wenye kuongoka. (2:157)
Umeionaje Makala hii.. ?
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w, sehemu ya 5. Hapa utajifunza kuhusu kuzaliwa kwa Mtume.
Soma Zaidi...Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a.
Soma Zaidi...Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a.
Soma Zaidi...Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.
Soma Zaidi...