Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo

Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo

Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.

KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO
Baada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Kiongozi ambaye alikabidhiwa mamlaka ya kukichimba upya kisima cha zamzam baada ya kufukiwa na watu kutoka kabila la Jurhum pindi walipoondoka Makkah.

 

Alisimama Abu Talib kumlea mtoto wa ndugu yake. Kwani huyu ndiye aliyekuwa mtoto mkybwa wa Abdul al-Muttalib.



Abu Talib alimpenda sana kijana wake zaidi ya anavyowapenda watoto wake. Mtume (s.a.w) alikuwa ni mwenyekuridhika kwa kile ambacho alikuwa akikipata.

 

Allah alimuongezea rizk mzee Abu Talib. Mzee huyu alimlea kijana wake Mpaka alipofika umri wa miaka arobaini. Watu walimpenda kijana Muhammad jinsi alivyokuwa na tabia njema na uaminifu.



Watu wa Makkah walikuwa wakiomba mvua kupitia utukufu wake. Imesimuliwa kutoka kwa Ibn ‘Asakir kuwa Jalhamah bin Arfuta kuwa amesema nilifika Makkah wakati ambao kulikuwa hakuna mvua, Maquraish wakatoka kumueleza mzee Abu Talib kuwa awaombee mvua.

 

Basi akatoka akiwa na kijana chake na akamsimamisha pembeni ya ukuta wa al-kabah kisha akaomba dua. Kwa hakika kulikuwa hakuna mawingu lakini ghafla mawingu yakajikusanya kutoka huku na kule na hatimaye mvua ikanyesha

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views: 4035

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 ai web app     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Mbinu za Da’wah Alizotumia Nuhu(a.s)

Katika kufikisha ujumbe huu kwa watu wake Nuhu(a.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa jihad katika kusimamisha uislamu katika jamii

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)

Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a.

Soma Zaidi...