Umuhimu wa KusimamishaSwala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.
Umuhimu wa Kusimamisha
Swala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.a) tuliyoirejea mwanzoni, kusimamisha swala ni nguzo ya pili ya nguzo za Uislamu. Katika kuonyesha umuhimu wa kusimamisha nguzo hii Mtume (s.a.w) amesema: Swala ndio nguzo kubwa ya Dini (Uislamu) mwenye kusimamisha swala amesimamisha dini (Uislamu) na mwenye kuiacha swala amevunja Dini .(Uislamu)
Katika Hadithi nyingine, amesimulia Jabir (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: Tofauti yetu sisi (Waislamu) na ukafiri ni kuacha swalah. (Muslim) Pia Mtume (s.a.w) amesema: Tofauti iliyopo kati yetu (Waislamu) na wengine (wasiokuwa Waislamu) ni swala (Ahmad, Abu Daud, An-Nasai, Tirmidh)
Kutokana na hadithi hizi, tunajifunza kuwa mtu ambaye hasimamishi swala, hatakama anajiita Muislamu si Muislamu bali ni kafiri kama makafiri wengine. Anakuwa kafiri kwa sababu amekanusha amri ya Allah iliyowazi kama inavyobainika katika aya zifuatazo: Waambie waja wangu walioamini, wasimamishe swala.(14:31) Basi simamisheni swala, kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi. (4:103) Na waamrishe watu wako kuswali (kusimamisha swala) na uendelee mwenyewe kwa hayo... (20:132).
Tukumbuke kuwa hawi Muumini yule anayekuwa na hiari katika kutekeleza amri ya Allah na Mtume wake kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo: Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi. (33:36).
Umeionaje Makala hii.. ?
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.
Soma Zaidi...Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza utaratibu wa kusherekea ifil fitir. Pia utajifunza sunnah zinazoambatsns na idil fitir
Soma Zaidi...Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa.
Soma Zaidi...