Namna ya kuosha maiti hatua kwa hatua

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

  1. Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati ili kupitisha uchafu unaotoka tumboni.
  2. Pawepo na shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, kama hakuna uwekano chombo kiwepo cha kukingia uchafu unaotoka kwa maiti.

        -  Pia maiti inaweza kuoshewa bafuni au kwenye karo liliotengenezwa

                     kwa kazi hiyo.

 

  1. Maiti afunikwe na nguo moja kubwa yenye kupenyeza maji wakati wa kuosha.

 

  1. Maiti akalishwe juu ya kitanda usawa wa tobo na shimo (ufuo) na ainamishwe nyuma kidogo, kama ni mzito ni vizuri msaidizi wa muoshaji amuegemeze kwenye magoti yake.

 

  1. Muoshaji apitishe mkono wa kushoto kwenye tumbo la maiti na kuliminyaminya taratibu ili kutoa uchafu ndani.

 

  1. Amlaze chali na kuminyaminya tumbo lake kama ilivyo mara ya kwanza.

 

  1. Aikalishe tena na apitishe mkono wa kushoto chini akiwa amevaa kitambaa au gloves na kusafisha tupu mbili kwa maji safi. 

-   Kama hapaja takata, basi na avae gloves safi na ile chafu aitupe kwenye  

                       ufuo na asafishe tena kama mara ya kwanza mpaka patakate.

 

  1. Baada ya hapo, muoshaji afunge kitambaa safi kwenye kidole chake shahada na akichovye kwenye maji na kumswakisha maiti meno yote na kisha akitupe ufuoni.

 

  1. Muoshaji azungushe kitambaa kingine safi kidole chake kidogo mkono wa kushoto na kumsafisha nacho maiti tundu za pua kisha akitupe ufuoni.

 

  1. Asafishe kucha za maiti kwa kijiti safi na laini iwapo ni ndefu na chafu.

 

  1. Kisha amkalishe maiti na amtawadhishe kwa kufuata taratibu za kawaida za kutia udhu (kutawadha).

 

  1. Maiti akiwa amekalishwa, ataanza kumuoshwa kichwa akiwa ameinamishwa mbele kidogo.

- Kama nywele au ndevu ni nyingi zichanwe na kuoshwa kwa sabuni na

   maji mpaka zitakate.

            - Mwanamke mwenye nywele nyingi zisukwe mikia, na zilizong’oka 

              ziambatanishwe na sanda.

 

  1. Baada ya kuoshwa kichwa, maiti italazwa kwa ubavu wa kushoto na kuanza kuoshwa ubavu wa kulia, mbele na nyuma kwa pamoja kwa sabuni na maji safi mpaka itakate.

 

  1. Kisha itaoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyooshwa wa kulia.

 

  1. Baada ya makosho (maosho) haya mawili, la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, kosho la tatu la maji liwekewe karafuu na marashi ili kulegeza viungo (maungo) vya maiti.

 

  1. Baada ya makosho matatu haya, muoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza kama alikuwa mara tu baada ya kufa.

 

  1. Kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti, na baada ya hapo maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na kufunikwa kwa nguo kavu tayari kuvalishwa sanda (kukafiniwa). 
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1349

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana: