Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Sharti za Swala
Sharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Mambo haya ni:
1. Twahara.
2. Sitara.
3. Kuchunga wakati.
4. Kuelekea Qibla.
Zifuatazo ni nguzo za Swala:
1. Nia - dhamira moyoni.
2. Takbira ya kuhirimia (au Takbira ya kufungulia Swala).
3. Kusoma suratul-Fatiha.
4. Kurukuu.
5. Kujituliza katika rukuu.
6. Kuitidali (kusimama kutoka katika rukuu).
7. Kujituliza katika itidali.
8. Kusujudu.
9. Kujituliza katika sijda.
10. Kukaa kati ya sijda mbili.
11. Kujituliza katika kikao cha kati ya sijda mbili.
12. Kusujudu mara ya pili.
13. Kujituliza katika sijda ya pili.
14. Kukaa Tahiyyatu.
15. Kusoma Tahiyyatu.
16. Kumswalia na kumtakia rehema Mtume (s.a.w) na Waislamu.
17. Kutoa Salaam.
18. Kuswali kwa kufuata utaratibu huu (1 - 17).
Nguzo hizi za swala tunaweza kuzigawanya kwenye makundi manne:
(a) Nia.
(b) Nguzo za matamshi (visomo)
(c) Nguzo za vitendo.
(d) Kufuata utaratibu. Katika nguzo 18,
nguzo za matamshi ni hizi tano zifuatazo:
(i) Takbira ya kuhirimia swala.
(ii) Kusoma suratul-Fatiha (Al-hamdu).
(iii) Kusoma Tahiyyatu.
(iv) Kumswalia Mtume.
(v) Kutoa Salaam.
Nguzo zote zilizobakia, ukiacha nia na kufuata utaratibu ni nguzo za vitendo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani.
Soma Zaidi...Assalamu Alaykum Warahmatu-llah Wabarakaatuh Naomba kuuliza: Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini?
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya Twahara Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu
Soma Zaidi...Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala.
Soma Zaidi...Post hii itakujuza jinsi ya kiswali swala ya tahajudi. Pia utajifunza jinsi ya kuswali swala za usikubyaanibqiyamublayl
Soma Zaidi...Hii ni orodha ya watu ambao wanaweza kurithi malibya marehrmu.
Soma Zaidi...