picha

FAIDA ZA VITAMINI C NA UMUHIMU WA VITAMINI C MWILINI

Utafahamu faida za vitamini C mwilini pamoja na kujuwa umuhimu wa vitamini C

FAIDA ZA VITAMINI C NA UMUHIMU WA VITAMINI C MWILINI


FAIDA ZA VITAMINI C MWILINI


Kama tulivyokwisha kuona vyakula vya vitamini C kama vile papai, machungwa, mananasi, maembe, malimao na ndimu. Pia tuliona baadhi ya kazi za vitamini C ambazo ni kusaidia katika kuuwa kemikali mbaya mwilini, kuipa nguvu miili yetu ya kupambana na maradhi. Katika makala hii nitakwenda kukujuza umuhimu wa vitamin C katuka mwili wa kila kiumbe akiwemo binadamu.


Faida na umuhimu wa vitamini C
1.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye (scurvy): Haya ni maradhi ambayo hufanya mwili uweze kutoa damu kwenye mafinzi, mwili kuchubuka kwa urahisi, kuchelewa kupona kwa majeraha. Kusoma zaidi kuhusu ugonjwa huu pitia zaidi makala zetu.


2.Kulinda mwili zidi ya maambukizi na mashambulizi:
Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.


3.Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.


4.Kulinda miili yetu dhidi ya saratani (cancer):
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:
A. Vitamini C husaidia kuborsha afya na kuishi vyema kwa wagonjwa wa saratani
B. Vitamini C inaweza kuuwa seli zinazotengeneza uvimbe wa saratani


5.Husaidia kulind miili yetu dhidi ya maradhi yanayohusu mishipa ya damu na moyo (cardiovascular)


6.Husaidia kulinda miili yetu dhidi ya maradhi ya ubongo na kusahasahau




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 1657

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 web hosting     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

utaratibu wa lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula zaituni

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula zaituni

Soma Zaidi...
Naombakujua kujua Kama huu uyoga unasaidia kansa Kama kwawazee

Mpaka sasa hakuna dawa ya kuponyesha saratani wala kinga ya saratani. Hata hivyo vipo vyakula ambavyo vinakadiriwa kuwa hupunguza hatari ya kuweza kupata saratani. Je unadhani uyoga ni moja ya vyakula hivyo?

Soma Zaidi...
HOMA YA DENGUE, DALILI ZAKE, TIBA YAKE, CHANGO YAKE NA INA SABABISHWA (AMBUKIZWA) NA MBU GANI

Homa ya dengue hupatikana sana Afrika, Asia na baadhi ya maeneo ya Caribbean.

Soma Zaidi...
VINYWAJI SALAMA KWA MWENYE KISUKARI

Kuchaguwa vinywaji si jambo rahisi, lakini inabidi iwe hivyo kama una tatizo la kisukari. Je unasumbuka kujuwa vinywaji salama? makala hii ni kwa ajili yako, hapa tutaona vinywaji ambavyo ni salama kwa mwenye kisukari.

Soma Zaidi...