Nini maana ya twahara katika uislamu
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo
Maana Ya Twahara Katika Lugha Ya Kawaida:
Ni usafi na kuondosha uchafu au takataka za kihisia (kugusika) kama najsi ya mkojo au kinginecho, na za kidhahania kama kasoro (mapungufu) na maasi.
Kutwaharisha ni kusafisha, nako ni kupaweka mahala maalumu katika hali ya usafi. [Al-Libaab Sharhul Kitaab (1/10) na Ad-Durru Al-Mukhtaar (1/79)].
Ama kisharia (kitaaluma):
Ni kuondosha kinachozuia kuswali kama hadathi au najsi kwa kutumia maji (au kinginecho), au kuondosha hukmu yake kwa mchanga. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (1/12)].
Hukmu ya twahara:
Kutwaharisha najsi na kuiondosha ni jambo la wajibu ikiwa mtu atakumbuka na ataweza. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:
((وَثِيَابَكَ فَطَهِّر))
((Na nguo zako zitwaharishe)) [Al-Muddath-thir (74:4)]
Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala):
((أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ))
((Ya kwamba itakaseni Nyumba Yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu na wanaojitenga humo kwa ‘ibaadah, na wanaoinama na kusujudu)). [Al Baqarah (2:125)]
Ama kujitwaharisha na hadathi, hilo ni lazima ili ruhusa ya kuswali ipatikane kwa neno lake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
(( لَا تُقْبَلُ صَلَاةُ بغير طهور))
((Swalaah haikubaliwi bila ya wudhuu). [Swahiyh Muslim 224]
Umuhimu Wake:
1- Twahara ni sharti ya kusihi kwa sala ya mja. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((لَا تُقْبَلُ صَلَاةُ مَنْ أَحْدَثَ حَتَّى يَتَوَضَّأَ ))
((Haikubaliwi Swalaah ya mtu mwenye hadathi mpaka atawadhe)). [Imepasishwa na Al Bukhaariy (135), Muslim (225].
Kuswali na twahara ni kumtukuza Allaah. Na hadathi na janaba – ingawa si najsi zenye kuonekana – lakini hata hivyo ni najsi za kidhahania zenye kukifanya kilichoingiwa navyo kuonekana kichafu. Hivyo basi, kuwepo kwake huteteresha utukuzo kwa Allaah, na huenda kinyume na msingi wa usafi.
2- Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Amewasifu wenye kujitwaharisha. Anasema:
((إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ))
((Hakika Allaah Anawapenda wenye kutubia mara kwa mara na Anawapenda wenye kujitwaharisha)). [Al Baqarah 2:222]
Akawasifu watu wa Masjid Qubaa kwa Neno Lake:
((فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُواْ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ))
((Ndani yake kuna watu wanaopenda kujitwaharisha, na Allaah Anawapenda wenye kujitwaharisha)). [At Tawbah 9:108]
3- Kutojali au kutotilia maanani kujitakasa na najsi, ni moja kati ya sababu za kuadhibiwa watu makaburini. Imepokelewa na Ibn 'Abbaas akisema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita kwenye makaburi mawili akasema:
(( إِنَّهُمَا لَيُعَذَّبَانِ وَمَا يُعَذَّبَانِ فِي كَبِيرٍ، أَمَّا هذا فَكَانَ لَا يَسْتَنزه مِنْ بَوْلِهِ، ))
((Kwa hakika wawili (hawa) wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. (la kuwashinda kutekeleza au kujiepusha nalo). Ama huyu, alikuwa hajitakasi na mkojo wake)). [Abu Daawuud (20), An Nasaaiy (31-69), na Ibn Maajah (347) kwa Sanad Swahiyh].
Hivyo ni wajibu wetu kuwa twahara Kila wakati na kujiepusha na najisi ama kukaa na najisi. Tukutane katika post inayofuata update muendelezo wa Darsa hii.
help_outlineZoezi la Maswali
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu.
Soma Zaidi...Namna ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Sunnah za siku ya idi na utaratibu wa kusherehekea
Hapa utajifunza utaratibu wa kusherekea ifil fitir. Pia utajifunza sunnah zinazoambatsns na idil fitir
Soma Zaidi...Madhara ya riba kwenye jamii
Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba?
Soma Zaidi...