Wajibu kwa Maskini na Wasiojiweza
Kila Muislamu wa kweli anawajibika kuwahurumia wanaadamu wenziwe walio katika hali mbaya ya kiuchumi kiasi cha kushindwa kupata mahitaji muhimu ya maisha kama vile chakula, kivazi, makazi ya kuishi, Elimu sahihi ya msingi, na kadhalika. Muumini kwa mujibu wa Qur-an, pamoja na sifa ~nyingine, ni yule mwenye tabia ya kuwahurumia wanaadamu wenzake wasio na uwezo na kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi ya maisha kama vile chakula. Tunasoma katika Qur-an:
Hakika watu wazuri watakunywa kinywaji kilichochanganyika na kafuri. (Hiyo kafuri) ni mto watakaounywa waja, wa Mwenyezi Mungu; watautitirisha mtitiririsho (mzuri namna watakavyo). (Watu hao ni hawa) wanaotimiza wajibu (wao) na wanaoiogopa siku ambayo shari yake itaenea (sana). Na huwalisha chakula maskini na may atima na wafungwa, na hali ya kuwa wenyewe wanakipenda (chakula hicho). (Husema wenyewe katika nyoyo zao wanapowapa chakula hicho); "Tunakulisheni kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala shukurani. "Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu hiyo siku yenye shida na taabu." Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema nafuraha. (76:5-1 1)
Ukiipitia Qur-an utaona imerudiwa mara nyingi katika kuainisha waumini wa kweli na wacha-Mungu kuwa ni "wale wanaosimamisha swala na kutoa yale waliyoruzukiwa na Allah (s.w) kwa njia ya kuwasaidia wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada. Kinyume chake, tunajifunza katika Qur-an kuwa si muumini wa kweli yule asiyejali kuwahurumia wasio jiweza:
".Je, umemuona yule anayekadhibisha dini (asiye amini malipo ya akhera)? Huyu ni yule anayemnyanyasa yatima wala hajihimizi kuwalisha maskini." (107:1-3).
Umeionaje Makala hii.. ?
Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi.
Soma Zaidi...Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha
Soma Zaidi...