Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinafanya wajawazito kupata ugonjwa wa Bawasili, kwa sababu tatizo hili linawapa wakina mama wajawazito, kwa hiyo tutaona kwa nini wajawazito wanapatwa na tatizo hili sana.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kwamba akina mama wajawazito upatwa na tatizo hili hii nikwa sababu ya kukua kwa mtoto kutoka hatua Moja kwenda nyingine na hivyo na uzito wa mtoto kuongezeka.
2. Kuwepo kwa mkandamizo au uzito kuzidi.
Kwamba tulivyotangulia kusema kwamba mwanamke Mjamzito uongezeka uzito na mgandamizo sehemu ya haja kubwa kwa sababu ya kuwepo kwa uzito wa mtoto na ukuaji wa mwili wa kizazi ( uterus) Hali hii upelekea mgandamizo sehemu ya haja kubwa na kusababisha mishipa ya damu midogo midogo kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa kupasuka hali inayosababisha kuota kwa vinyama au uvimbe kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa inayoambatana na miwasho.
3. Tatizo lingine ni ulaji wa udongo.
Tunafahamu kabisa wakati wa ujauzito akina Mama ula vitu vingi mbalimbali pamoja na udongo kwa sababu ya kukosa madini ya chuma kwa hiyo ulaji wa udongo usababisha wajawazito kupata choo kigumu hali ambayo usababisha wajawazito kutumia nguvu kubwa wakati wa kujisaidia hali inayosababisha Mishipa midogo midogo kwenye sehemu za haja kubwa kupasuka na hatimaye kuota uvimbe na vinyama kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa.
4. Unywaji mdogo wa maji wakati wa ujauzito.
Kwa kawaida wakati wa ujauzito akina Mama wanapaswa kunywa maji ya kutosha kwa sababu ya faida mbalimbali kwenye mwili.ila Kuna baadhi ya akina Mama wakati wa ujauzito wanabagua sana vyakula hata na maji wengine hawataki kabisa kutumia hali inayosababisha choo kuwa kigumu na katika harakati za kutoa choo unaweza kukuta mishipa ya haja kubwa kupasuka na kusababisha kuota uvimbe na vinyama kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa.
5. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kunywa maji ya kutosha pamoja na kutoa taarifa yoyote endapo wataona mabadiliko yoyote mwilini Ili kuepuka na balaa hili la bawasili na pia choo kikiwa kigumu no vizuri kabisa kutumia mboga mboga za majani na dawa Ili kurainisha choo hicho
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Unaweza kutaka kujuwa je naweza kupata dalili za mimba baada ya siku nne toka ujauzito kutungwa? ama baada ya siku nne toka kushiriki tendo la ndoa. Makala hii itakwenda kujibu maswali haya na mengineyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo tunaweza kuzitumia ili kuwakinga watoto dhidi ya saratani, kama tulivyotangulia kusema kwamba saratani ya watoto mara nyingi Usababishwa na akina Mama hasa kwa sababu ya mtindo wa maisha wakati wa ujauzito kwa hiyo tun
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa akina Mama, tunajua wazi kubwa kuna faida kubwa za uzazi wa mpango kwa akina Mama pindi watumiapo njia hizi kwa uhakika zaidi.
Soma Zaidi...Maumivu wakati wa tendo la ndoa kitaalamu huitwa dyspareunia.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma kwa wanaoingia kwenye siku zao zaidi ya mara moja kwa mwezi.
Soma Zaidi...Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uhusiano uliopo kati ya Mama Mjamzito na kibofu cha mkojo.ni mwingiliano unaokuwepo ambao usababisha Mama kukojoa sana wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuepuka fangasi za ukeni, ni njia ambazo usaidia kuepuka madhara ya fangasi za ukeni.
Soma Zaidi...