picha

Aina mbalimbali za mimba kutoka.

Post hii inahusu zaidi aina mbalimbali za mimba kutoka, hizi ni jinsi mimba inavyoonyesha dalili za kutoka na nyingine zinaweza kuonyesha dalili Ila kwa sababu ya huduma mbalimbali za kwanza hizo mimba zinaweza kudhibiiwa na mtoto akazaliwa.

Aina mbalimbali za mimba kutoka.

1. Kama tulivyoona kwenye utangulizi tunaweza kuona aina mbalimbali za mimba kutoka na dalili ambazo ujionyesha kwa namna Moja au nyingine, kwa hiyo zifuatazo ni aina mbalimbali za mimba kutoka.

 

 

 

2. Kuna mimba ambazo zinatishia kutoka ( threaten abortion).

 Hii ni aina mojawapo ya mimba kutaka kutoka ila mama akiwahi anaweza kusaidiwa  au kuzuia mimba hiyo isitoke , kwa kawaida mimba ya aina hiyo huwa na miezi sita, ikiwa mama ni mjamzito na akaona damu zinatoka ila kwa kawaida inakuwa ni ndogo kwa siku kama Ile inayotoka siku za mwezi au inawezekana ikawa ndogo yake na pia damu uendelea kutoka kidogo kidogo na panakuwepo na maumivu yasiyo ya Kawaida au kwa wanawake ambao wameshajifungua ni kama maumivu ya uchungu, ikiwa mama anaona hali kama hiyo awai hospital ni mimba Inayotishia kutoka ,  Mama akipata huduma haraka anaokoa  maisha ya   mtoto, mtoto anaendelea kukua na akafikia siku ya kuzaliwa  na anazaliwa kawaida tu.

 

 

 

 

 

2. Mimba ambayo inataka kutoka na hata juhudi zozote zikitolewa ni kazi Bure, kwa kitaamu huiitwa inevitable pregnant.

Hii ni aina ya mimba ambayo Ina dalili za kutoka kw  hata juhudi gani ziwekwe ni kazi Bure mimba ni lazima itoke tu,hii aina ya mimba ambayo ni tofauti na tuliyomaliza kuongelea hapo awali, kwa sababu mama anakuwa anatokwa na damu nyingi yakiandamana na maumivu yasiyo ya Kawaida na pia Mama anakuwa na maumivu makali ya mgongo na katika kumwangalia unaona kama mimba imeshaharibika , kwa hiyo mjamzito akiona dalili kama hii ni vizuri kwenda hospital Moja kwa Moja , kwa kawaida mimba za hivi huwa ni chini ya miezi sita, kwa hiyo jamii na wote waliomzunguka wanapaswa kumsaidia mama Ili aweze kwenda kupata matibabu kwa sababu kama mimba ikitoka akiwa nyumbani ni hatari kwa sababu Kuna vipande vipande vinaweza kubaki na kusababisha madhara makubwa kwa Mama.

 

 

 

 

 

3. Mimba ambayo imeshatoka ila Kuna vipanda vipande vimebaki.( Kwa kitaamu huiitwa incomplete abortion)

hii  ni aina ya mimba ambayo ikitoka Kuna baadhi ya vipande vipande vinabaki ndani ya mfuko wa uzazi wa Mama,au kwa wakati mwingine sehemu ya kondo la nyuma ubaki, hali hii utokea kwa akina Mama ambao dalili za kutoka kwa mimba utokea wakiwa nyumbani ila kwa sababu ya mazingira au matatizo ya kiuchumi ukazana au kujikaza na kuacha mimba ikatoka wakiwa nyumbani hali inayosababisha baadhi ya vipande kubaki na hali hii usababisha mama kuumia tumbo au pengine kuwepo kwa maambukizi ambayo kwa kitaamu huiitwa sepsis, kwa hiyo kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mama ingawa mtoto ameshaondoka, kwa hiyo jamii inapaswa kujua na kuelewa kwamba pindi tu Mama anapobeba mimba maandalizi yanapaswa kuanza hasa ki uchumu kwa kutunza Hela ndogo ndogo Ili kuweza kuokoa maisha ya Mama na mtoto kwa sababu chochote kinaweza kutoka wakati wa ujauzito, kwa hiyo akina Mama wanapatwa na hali hii kwa sababu hawana ela ya kukidhi matibabu endapo mimba zikitoka wakiwa nyumbani hali inayopelekewa mimba kutoka kienyeji na vipande vipande vinabaki.

 

 

 

 

 

4. Mimba inayotoka ni vipande vipande vikatoka kabisa na kuisha.

Hii ni tofauti na mimba ambayo tumetoka kujadili aina hii ya mimba kwa kitaamu huiitwa complete abortion, Dalili za kutoka kwa mimba zote zinakuwepo kama vile maumivu makali ya tumbo, maumivu ya mgongo na kuwepo kwa uchungu, na hatimaye mimba utoka na inapotoka kila kitu kinatoka na hakuna kinachobaki na damu pia uacha kuvuja ndani ya mda mfupi, ila ubaki maumivu ya Kawaida tu ,kwa hali hii hata mama akiwa nyumbani hakuna shida kwa sababu kila kitu kimetoka ila ni vizuri kabisa kujihakikishia kama kila kitu kimetoka kwa kuwaona wataalamu wa afya au kwenda kituo cha afya kilicho karibu kwa ajili ya uangalizi. Kwa hiyo ni vizuri kabisa jamii inayomzunguka Mama kumpa ushirikiano wa kutoka katika hali ngumu kama hii.

 

 

 

 

 

5. Kuna mimba ambapo mtoto anafia tumboni akiwa chini ya miezi sita.

Hii uitwa aina mojawapo ya mimba kutoka kwa sababu mimba inakuwa chini ya miezi sita na mtoto anafia tumboni, hali hii utokea kwa sababu mbalimbali kama vile, labda maambukizi ya magonjwa kama vile kaswende, kisonono, malaria, UTI na maambukizi mbalimbali, au labda Mama kapigwa na kusababisha mtoto kufia tumboni, mimba za aina hii huwa na dalili mbalimbali kama vile mtoto kuhindwa kucheza, mapigo ya mtoto kutosikika na mama akilalia ubavu na mtoto uelekea huko na akibadilisha ubavu mwingine na mtoto ulalia huko hali hii umfanya Mama kuwa na wasiwasi, kwa hiyo Mama akiona dalili za hivyo ni vizuri kabisa kuwahi hospital Ili kuokoa maisha yake.

 

 

 

 

 

 

6. Mimba kutoka Kuna sababu mbalimbali ambazo usababisha kwa hiyo mama aikona dalili yoyote ya mimba kutoka ni vizuri kabisa kuwahi kituo cha afya ili kupata matibabu zaidi na pia ndugu waliomzunguka wanapaswa kumpatia ushirikiano nzuri Ili kuweza kumsaidia Mama akiwa katika hali hii.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views 3264

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 ai web app     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Fahamu siku za kubeba mimba na zisizo za kubeba mimba.

Posti hii inahusu zaidi siku za kubeba mimba na zisizo za kubeba mimba , tunapaswa kujua hivi Ili kuweza kupanga uzazi na kuepuka njia ambazo ni hatarishi kwa afya zetu.

Soma Zaidi...
utaratibu wa lishe kwa Mjamzito, Vyakula anavyopasa kula mjamzito

Ni vyakula gani anapasa kula mjamzito, na utaratibu mzima wa lishe kwa wajawazito

Soma Zaidi...
Ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango.

Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango.

Soma Zaidi...
Malezi ya mtoto mchanga na mama mjamzito

Post hii itakwenda kukuletea mambo kadhaa yanayohusiana na malezi bora ya mama mjamzito na mtoto mchanga

Soma Zaidi...
anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu

Abali mkuu Nina mdogo wangu anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu na zenye kutisha uume wake nao umekuwa unakama mabaka umebabuka aisee nime angaika Sana kumtibia mpaka nakata tamaa

Soma Zaidi...
Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa Wanaume

Posti hii inazungumzia Faida, hasara, na madhara ya Kufunga kizazi kwa Wanaume.

Soma Zaidi...