picha

Sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa

Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa.

Sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa.

1. Sababu ya kwanza vifaa vinavyotumika kuzalisha watoto.

Kuna wakati mwingine vifaa vinavyotumika kuzalisha watoto usababisha kuchubuka kwa mtoto inawezekana kabisa ni kwa kuchubuka kwa ndani au kuchubuka kwa ngozi ya nje, Kuna Kipindi mtoto anakuwa ameshatoa kichwa ila kutoka nje huwa ni shida na hata kama mama akisukuma kwa namna gani mtoto hawezi kutoka hali inayosababisha  vifaa mbalimbali kutumika Ili kuweza kumtoa mtoto nje na kuokoa maisha ya mtoto na Mama kwa hiyo katika kimvuta mtoto atoke usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa kwa hiyo ni vizuri kabisa wataalamu wa afya na wahudumu wa mtoto aliyevutwa kwa kutumia vyuma kuangalia mara kwa mara Ili kuweza kugundua kama michubuko ni ya ndani au ya nje na kuweza kutumia matibabu.

 

2. Pia michubuko utokea mara nyingi kwa watoto wanaozaliwa kwa kutanguliza matako, kwa kawaida mtoto anapaswa kutanguliza kichwa ikitokea mtoto akatanguliza matako, au miguu usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa,kwa sababu matako na miguu uweza kuzaliwa ila Kuna Kipindi mabega na mikono ushindwa kutoka, katika kupambana ili kuweza kutoa mikono na mabega au pengine kichwa usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa, na pia sio michubuko tu kwa wakati mwingine ulemavu wa mikono na mabega uweza kutokea kwa watoto, kwa hiyo kwa akina mama wanaojifungua ikitokea mtoto alikuwa ametanguliza matako au miguu na akazaliwa kwa shida kwa kupambana ni vizuri kabisa kuangalia mabadiliko yoyote na kumwambia wataalamu wa afya Ili kuweza kuepuka madhara mengine zaidi.

 

3. Mtoto kutanguliza mabega.

Kuna wakati mwingine mtoto anaweza kutanguliza kichwa na kichwa kikazaliwa ila mabega yakakwama kwenye mfupa wa mama ambao kwa kitaamu huiitwa pubic bone, kwa hiyo katika kupambana kuzalisha mabega Ili mtoto atoke usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa, kwa hiyo ni vizuri kabisa kujua dalili za mtoto aliyetanguliza mabega Ili kuweza kutafuta mbinu za kuzalisha mama huyo au kutafuta wataalamu zaidi, na dalili ambazo ujitokeza ni kama zifuatazo.

  1. Mtoto anaweza kutoa kichwa vizuri kabisa ila badala ya kuendelea kawaida kichwa uanza kurudi tena nyuma kilipotoka ,kwa wakunga dalili hii uinesha kwamba mabega bado hayajatoka.
  2. Pia kuzunguka kwa mtoto upungua ambapo kitendo hiki kwa kitaamu huiitwa decreasing of restitution, kwa kawaida mtoto akitoa kichwa uzunguka Ili kuweza kuruhusu na bega litoke ila kwa sababu mabega hayajatoka mtoto hawezi kuendelea na kuzunguka tena.

Mama huwa na wasiwasi mkubwa kuliko kawaida na pia uhisi kitu ambacho sio cha Kawaida kwa hiyo kwa wahudumu wa afya ni vizuri kabisa kuwa karibu na mama Ili kuweza kumweka mama kwenye hali nzuri na ya kwamba kila kitu kitakuwa sawa.

 

4.Kichwa cha mtoto kutolingana na kiuno cha mama kwa pale mtoto anapopaswa kupitia.

Kwa kawaida kichwa cha mtoto ni lazima kabisa kulingana na kiuno cha mama kwa pale mtoto anapopaswa kupitia, hali ambayo usababisha mtoto kutumia nguvu nyingi Ili kutoka nje ,hali hii kwa kitaamu huiitwa disproportionate pelvic, kwa hiyo kabla ya mama kujifungua ni lazima kujua hali halisi ya mtoto anapotaka kujifungua kama anaweza kupita au hawezi kupita kwa kufanya hivyo tunaweza kuepuka matatizo mbalimbali kwa watoto kama vile kuchubuka na ulemavu mwingine kama huo.

 

5. Na tatizo jingine mama kukaa kwenye Kipindi cha kujifungua kwa mda mrefu , yaani kwa kitaamu huiitwa prolonged labor.

Ni hali ambayo mama huwa na uchungu wa mda mrefu na pia anakaa kwenye uchungu kwa mda huo inawezekana ukawa mchache ule ambao haiwezekani mtoto kuzaliwa, kwa hiyo mtoto uchoka na kwa pengine usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa,

 

6. Vile vile Kuna hali ya uchungu kuwa mkali na kichwa cha mtoto hakishuki chini, kwa kitaamu huiitwa obstruction labour.

Hii ni Sina ya labor ambapo uchungu unakuwepo wa kutosha lakini kichwa cha mtoto hakishuki, kwa sababu uchungu upo na mtoto anapambana kutoka ila kichwa hakishuki kwa hiyo hali hiyo usababisha kuchoka kwa mtoto na pia mtoto uweza kupata michubuko,hali hii pia usababisha mama kupasuka kizazi na kusababisha kupoteza mtoto na pia kuleta matatizo kwa mama na pengine kizazi kikisha pasuka usababisha kutolewa hali hii inaweza kumfanya mama kushindwa kupata naomba ya watoto aliokusudia kupata.

 

7. Pengine hali inayosababisha kupata michubuko kwa watoto ni pamoja na uchungu kuwa mkubwa zaidi na WA mda mfupi, kwa kitaamu huiitwa precipitate labor.

Ni aina ya uchungu ambao utokea kwa akina mama kwa kawaida utokea kwa mda mfupi na pia mama uweza kujifungua kwa mda mfupi huo, kwa kawaida uchungu huo utumia masaa matatu tu, na pia mtoto uweza kuzaliwa, kwa hiyo mtoto ni kama vile anatoka kwa spidi kubwa na kujibamiza kwenye mifupa mbalimbali ya kiuno cha mama na kusababisha hali ya  michubuko.

 

6. Kwa hiyo akina mama wanapaswa kuwa makini katika Kipindi cha ujauzito kwa sababu Kuna vitu vingine ambavyo usababisha madhara kwa watoto na vile vile akina mama wanapaswa kuhudhuria Kipindi cha mahudhulio yote wakati wa ujauzito Ili kuweza kugundua dalili za hatari na mambo ambayo usababisha michubuko na matatizo mengi mbalimbali .

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views 2621

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 web hosting     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Njia juu zinazosababisha kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi

Post hii inahusu zaidi njia za kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.

Soma Zaidi...
Upungufu wa maji

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa maji mwilini

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu vitamini K na kazi zake mwilini

vitamini k ni moja katika vitamini vinavyoitajika sana mwilini. Je unazijuwa athari za upungufu wa vitamini k mwilini?

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu protini na kazi zake mwilini

Tunahitaji kuwa na protini mwilini. Kuna baadhi ya makundi ya watu wanahitaji protini zaidi. Je unawajuwa hao ni kina nana?, na je unauwa kazi za protini mwilini na athari za upungufu wake? endelea na makala hii.

Soma Zaidi...
Vipi utaepuka maumivu ya kichwa ya mara kwa mara?

maumivu ya kichwa ni moja ya dalili za kiafya ambazo huashiria hali isiyo ya kawaida. hata hivyo maumivu ya kichwa yanaweza kutokea hata kama sio mgonjwa. Hapa nitakuletea sababu zinazopelekea kuumwa na kichwa mara kwa mara.Maumivu

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka

Soma Zaidi...