Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema.
Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema. Ukikutana na mtu huyu usimkimbie. Kwanza msogelee karibu kisha hakikisha kama yupo hai ama laa. Kama yupo hai, kwanza angalia kama utaweza kupiga simu kituo cha afya, ama mtaalamu wa afya. Hakikisha maamuzi haya na utekelezwaji unafanyika haraka bila ya kuathiri hali ya mgojwa.
Baada ya kujiridhisha na maamuzi uliyochukuwa unaweza kuanza huduma ya kwanza, ya kumsaidia mgonjwa asiyepumua aweze kupumua. Hapa tutafanya huduma ya kwanza itambulikayo kama CPR. Hii ni huduma ya kwanza inayohitaji umkini wa hali ya juu. Lakini kwa ambaye hafahamu chochote kuna namna anavyotakiwa kufanya
1.mlaze mgonjwa kichalichali juu ya sehemu iliyo ngumu, isiwe sehemu inayobonyea kama kitandani
2.Punguza nguo zilizopo kifuani kwake, na kama ni mwanaume unaweza kumvua shati kabisa.
3.Bidua kidogo kichwa cake
4.Weke mkono wako wa mmoja juu ya mwengine, kisha iweka katikati ya chuchu za mgonjwa.
5.Anza kumbonyeza kifua chake kwa wastani wa mibonyezo 100 paka 120 kwa dakika moja. Yaani karibia mibonyezo miwili kwa sekunde.
6.Hakikisha unabonyeza kwa nguvu mpaka uone kifua cha mgonjwa kinapanda na kuchuka kutokana na mibonyezo yako.
7.Usizidishe nguvu kupitiliza ukavunja mifupa ya mgonjwa.
8.Enelea kufanya hivi mpaka utakapoona mgonjwa anweza kupumua.
9.Muwahishe mgonjwa kituo cha afya baada ya kuanza kupumua.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi faida za seli. Seli ni chembechembe hai za mwili ambazo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya DTP au DPT ambayo Inazuia magonjwa ya Donda Koo, Pepopunda na kifaduro.
Soma Zaidi...Katika vyakula tunaposema wanga tunamaanisha virutubisho ambavyo hupatikana kwenye vyakula. Hivi husaidia sana katika kuifanya miili yetu iwe na nguvu.
Soma Zaidi...Pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu kitaalamu huitwa bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na michubuko sugu mwilini kwenye mirija yake ya kupitisha hewa. Hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea utaratibu wa maisha kwa aliye athirika
Soma Zaidi...Hata kama mtu atakuambbia usile vyakula yenye mafuta bado itahitajika kula tu. Kuna mafuta na fati je unajuwa utofauti wao. Ni zipi kazi zao mwilini? Endelea na makala hii
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu.pua ni mlango wa fahamu ambao uhusika na kupumua.
Soma Zaidi...Tunahitaji kuwa na protini mwilini. Kuna baadhi ya makundi ya watu wanahitaji protini zaidi. Je unawajuwa hao ni kina nana?, na je unauwa kazi za protini mwilini na athari za upungufu wake? endelea na makala hii.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo maradhi huambukizwa
Soma Zaidi...