Dalili za upungufu wa homoni ya projestron

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.

Dalili za upungufu wa homoni ya progesterone.

1. Kutokwa kwa mimba.

Kwanza kabisa Mama akiwa na upungufu wa homoni ya progesterone anaweza kutoka mimba kwa sababu homoni hii ni msaada mkubwa katika makuzi ya mimba kama homoni hii ni ndoo kutoka kwa mimba ni kugusa.

 

2.pre menstruation syndrome.

Hali hii inamkumba mwanamke wiki Moja Hadi mbili  kabla ya kuona siku zake za mwezi  Mama anakuwa na uchovu, miwasho sehemu za Siri, vipele vyekundu au vyeusi, pamoja na mabadiliko ya mood kama vile hasira au kuwa na furaha kupita kiasi.

 

3. Kuongezeka uzito kwa ghafla na kuwa na wasiwasi,Kuna kipindi ambapo Mama anaweza kuongezeka uzito kwa ghafla na kuwa na wasiwasi usio wa kawaida hali hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kidogo cha homoni ya progesterone.

 

4. Maumivu ya uvimbe  kwenye maziwa,

Kuna wakati mwingine mama anakuwa na maumivu yanayoambatana na uvimbe pamoja  kwenye matiti hali hii utokana kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kidogo cha homoni ya progesterone na kiwango kikubwa cha homoni ya estrogen.

 

5. Kupata kizungu zungu mara kwa mara.

Kwa kawaida Mama mwenye tatizo hili huwa anapatwa na kizungu zungu mara kwa mara kwa sababu ya kutokuwepo kwa usawia katika homoni ya progesterone kwa kiwango cha kutosha.

 

6. Vipele vyekundu na chunusi hasa usoni  na ngozi kuwa na mafuta mengi na ya kuzidi kiasi .

 

7. Kuwepo kwa maumivu ya kichwa ya mara Kwa mara hasa kwa akina Mama wlio kwenye wakati wa kujifungua.

 

8. Kupoteza kumbukumbu na kuwepo kwa uzito wa kufikilia.

Kwa wakati mwingine mama anaweza kupoteza kumbukumbu mara kwa mara na kuwepo kwa uzito wa kufikilia mambo.

 

9. Kuwepo kwa ugumba.

Kwa sababu kazi ya homoni ya progesterone ni kusababisha uchevushaji wa mayai na pia kusaidia katika uzalishaji pamoja na kutungwa kwa mimba kwa hiyo homoni hii ikikosa inaweza kusababisha hali ikawa mbaya zaidi na Mama au dada kupata ugumba.

 

10. Pamoja na Daili tulizoziona si dalili zote utokea kwa sababu ya kukosa kwa homoni ya progesterone ni vizuri kabisa kupima au kuwaona wataalamu wa afya endapo umepatwa na tatizo hili hasa kutoka mimba au ugumba unaoendana na dalili kama tulivyoziona hapo juu.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/03/Sunday - 09:19:44 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1994


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-