Sababu za kutokea uvimbe kwenye kizazi.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi,kwa kawaida tumesikia akina mama wengi wanalalamika kuhusu kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi na wengine hawajui sababu zake kwa hiyo sababu zifuatazo ni za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.

Sababu za uvimbe kwenye kizazi.

1.kuongezeka kwa vichocheo vya homoni ambazo ni progesterone homoni na oestrogen homoni.

Hizi homoni kwa kawaida zinakuwepo kwenye mwili ila ikitokea zikaongezeka zaidi zinaweza kuleta madhara ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi kwa hiyo hizi homoni zinapaswa kuwepo kwa kiwango maalumu sio kuzidi sana.

 

2. Kuwepo kwa ujauzito.

Kwa kawaida ujauzito uweza kusababisha kuwepo kwa uvimbe kwa sababu wakati wa kujifungua kuna uchafu mwingine ukibaki uweza kusababisha kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.

 

3. Uzito na unene kupita kiasi.

Kwa wakati mwingine kuna kiasi cha uzito au unene kupita kiasi kwa sababu mwili ni kama umejaza vitu mbalimbali na ambavyo havina mazoezi kwa hiyo uendelee ujirunda ndani na hatimaye kusababisha uvimbe kwenye kizazi.

 

4. Kuwepo kwa mfumo usio sawa wa mishipa ya damu.

Kitendo cha kuwepo kwa mfumo usio sawa wa mishipa ya damu Usababisha uvimbe kwa sababu kwa wakati mwingine damu haiwezi kusafili kutoka sehemu moja kwenda nyingine na hali hii Usababisha uvimbe kwenye kizazi.

 

5. Sababu za kuridhi.

Kuna familia nyingine huwa na tatizo hili la kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi na kufanya kila mtoto anayezaliwa kwenye familia hiyo kuwa nao hii ni kwa sababu familia hiyo inakuwa na uzalishaji wa homoni zisizofaa na kusababisha uvimba kwa kizazi.

 

6. Lishe isiyofaa 

Kuwepo kwa lishe isiyofaa nalo ni tatizo la kufanya uvimbe kwenye kizazi kwa sababu tunajuwa wazi kuwa chakula ni dawa kwa hiyo bila lishe ya muhimu kila ugonjwa utakushambulia. Kwa hiyo tunapaswa kutumia vyakula vya kutosha na vyenye lishe bora



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/07/Monday - 09:04:44 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1658


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-