Posti hii inahusu zaidi Dalili za uvimbe kwenye kizazi,hizi ni Dalili ambazo ujitokeza kwa akina mama ambao wana uvimbe kwenye kizazi kwa hiyo endapo mama ameona Dalili kama hizi anapaswa kuwahi hospitali mara moja kwa uangalizi zaidi.
Dalili za uvimbe kwenye kizazi.
1. Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.
Hii ni Dalili mojawapo ambayo inaweza kujitokeza kwa Mama au msichana ambaye hajaolewa, ikitokea damu ikaongezeka kupita kiasi kusiko kwa kawaida wakati wa hedhi ni Dalili mojawapo ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.
2. Maumivu makali wakati wa hedhi.
Kwa wakati mwingine maumivu yanaweza kuwa makali kuliko kawaida au mtu mwingine anakuwa hana maumivu wakati wa hedhi ila ikitokea shida hizi ya kuwepo kwa uvimbe maumivu yanaanza kuwepo.
3. Kuvimba miguu.
Nayo ni Dalili ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi utaona mama au mdada yeyote amevimba miguu kwa hiyo anapaswa kwenda hospitalini kupima.
4. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Kwa wenye matatizo ya kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi wanapatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa na kwa hiyo huwa hawana furaha wakati wa tendo ila ni maumivu tu.
5. Kuwepo kwa gesi tumboni .
Au kwa wakati mwingine mtu ujisikia kama amevimbiwa na tumbo linakaa limevimba kama vile linakuwa na gesi.
6. Kupata choo kigumu au kufunga choo kabisa .
Kwa kawaida mtu mwenye matatizo ya kuwepo kwa uvimbe huwa na matatizo ya kukosa choo na huko anakuwa anakula chakula kawaida na kwa wakati mwingine anahisi kwenda haja kubwa ila choo kigumu nakuwa kama kigumu sana.
7. Maumivu n kwenye mgongo.
Hili tatizo uwapata wanawake walio wengi na udhani ni mgongo inauma lakini baada ya kufanyiwa upasuaji na kutoa uvimbe kwenye kizazi maumivu haya hayatokeagi tena.
8. Maumivu kwenye miguu na miguu kuvimba.
Kwa wakati mwingine Maumivu yanakiwepo kwenye miguu na miguu uanza kuvimba .
9. Kuwepo kwa ugumba au uzazi wa shida.
Kwa wakati mwingine wa mama wengi wanaangalia kutafuta watoto na hawapati shida kubwa inakuwa kwenye kizazi na wakifanyiwa upasuaji wanaweza kupata watoto.
10. Maumivu kwenye nyonga.
Kwa wakati mwingine mama huwa anapata maumivu makali kwenye nyonga ambayo umfanya mama kulalamika kila wakati.
11.mimba kutoka mara kwa mara.
Ikitokea mama kabeba mimba, hizo mimba utoka mara kwa mara na wakati mwingine mama anaweza kuangaika mpaka pale atakappgundua tatizo.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza siku nzuri kushoriki tendo la ndoa kupata ujauzito, dalili za siku hiyo na kuitafuta kwa mahesabu
Soma Zaidi...Posti hii zaidi kazi ya Dawa ya metronidazole katika kutibu Minyoo, ni aina ya Dawa ambayo imetumiwa na watu wengi wakaweza kupona na kuepukana na minyoo. Zifuatazo ni baadhi ya kazi za metronidazole.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea namna mwanamke anavyoweza kupata Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa watoto, sio akina Mama peke yao wanaofaidika na uzazi wa mpango vile vile na watoto wanafaidika na uzazi wa mpango kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Point hii inahusu zaidi mbinu za kupunguza Kichefuchefu hasa kwa wagonjwa na watumiaji wa madawa mbalimbali yanayoweza kusababisha kichefuchefu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kugundua tatizo lake na kutoa msaada pale penye uhitaji.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye Matiti kwa Mama mjamzito, hali hii utokea pale ambapo mama akibeba mimba Kuna mabadiliko kwenye Matiti kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kama kuna Maambukizi yoyote kwenye kitovu cha mtoto mdogo, kwa kawaida kitovu cha mtoto kama kiko vizuri kinapona kwa mda mchache na kinakauka mapema iwezekanavyo bila kuwa na tatizo lolote ila kama kuna Dal
Soma Zaidi...