Vyanzo vya kuharibika kwa mimba ya miezi kuanzia 0-3

Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuharibika kwa mimba kuanzia miezi zero mpaka miezi mitatu, kwa sababu hii ni miezi ya kwanza kabisa Kuna sababu au vyanzo vya kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki.

Vyanzo vya kuharibika kwa mimba kuanzia miezi zero mpaka miezi mitatu.

1. Sababu ya kwanza ni kitendo cha homoni kutokuwa sawa kwa sababu katika kipindi hiki ni wakati ambao homoni nyingi uwepo Ili kuhakikisha kazi mbalimbali zinafanyika kama vile kutengeneza kondo la nyuma kama homoni haziko sawa mimba inaweza kutoka.

 

2. Sababu za vinasa Saba 

Hizi ni sababu ambazo uchangiwa na wazazi wenyewe anaweza kuwa baba au mama , ndio usababisha mimba kutoka kwa kipindi hiki.

 

3. Matumizi ya dawa kiholela.

Kuna tabia ya kutumia dawa kiholela bila kupata ushauri wa daktari katika kipindi hiki hasa akina Mama wengi uchanganya madawa Kuna madaw ya kienyeji na ya hospital hasa matumizi ya madawa ya malaria , usababisha mimba kutoka.

 

4. Maambukizi ya magonjwa.

Kuna tabia ya maambukizi ya magonjwa kama vile kisonono, kaswende na maambukizi kwenye mlango wa kizazi kama maambukizi haya hayakugundukika mapema na kitibiea usababisha mimba kutoka.

 

5. Pia Kuna maambukizi kwenye mfuko wa uzazi.

Kuna wakati mwingine maambukizi kwenye mfuko wa uzazi usababisha mimba kutoka kwa sababu unakuta sehemu mbalimbali za kizazi zimeshambuliwa hali ambayo usababisha mimba kutoka.

 

6. Kuwepo kwa uvimbe.

Pia na hili ni Mojawapo ya tatizo kwa Sababu kama kwenye mfuko wa uzazi Kuna uvimbe mama hawezi kubeba mtoto kwenye mfuko huo kwa sababu utakuta uvimbe huo unashika sehemu mbalimbali ambapo mtoto anapaswa kuwepo.

 

7. Uvutaji wa sigara kupita kiasi na unywaji wa pombe kupita kiasi usababisha mimba kutoka kwa sababu ya kuwepo kwa nicotine na kemikali mbalimbali za pombe.

 

8. Kufanya kazi ngumu na kubeba mizigo mizito.

Pia kazi ngumu Nazo usababisha kutoka kwa mimba kwa sababu ni vigumu kabisa mimba kustahimili kwa mama anayefanya kazi hizo ngumu.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/21/Thursday - 07:06:34 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1155


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-