Sababu za kushuka surat al Zilzalah
surat Zalzalah ni sura ya 99 katika mpangilio wa Quran, na ina aya 8. Sura hii imeteremshwa Madina ila pia kuna kauli zinathibitisha kuwa ni ya Makkah. Katika hadithi iliyopewa daraja la hassan na Imam Tirmidh Mtume S.A.W amesema kuwa kusoa surat Zilzalah
Asbab Nuzul Surat Zilzalah
Ama kuhusu sababu za kushuka sura hii, hakuna nukuu za kutosha kuonyesha hasa tukio ambalo lilitokea hata sura hii ikashushwa. Hata hivyo kutokana na maelezo ya Sa'id bin Jubair ni kuwa baada ya kushuka aya ya 8 ya surat Al insan watu walidhani kuwa wak=liotoa sadaka kidogo sana hawatalipwa na wengine wakadhani kuwa dhambi ndogo wanazozifanya hawataadhibiwa, hivyo Allah akashuka aya 7 na 8 katika surat al zilzalah.
Kutokana na maelezo Maelezo ya Sura hii kuwa ukifanya dhambi iwe ndogo kiasi gani utalipwa malipo yake, na ukifanya wema mdogo kiasi gani pia utalipwa. Ama kuhusu wema kuna maelezo mengine zaidi ni kuwa Quran inasibitisha kuwa wema hulipwa kwa marakumi zaidi ama zaidi ya hapo. Yaani mfano umetenda wema mmoja, basi Allah atazidisha kwa kumi malipo yake. Na huwenda akazidisha zaidi ya hapo hata mara mia saba kama Surat Al Baqarah inavyoeleza ama zaidi na zaidi.
Imesimuliwa Kutoka kwa Abdallah Inb Umar kuwa wakati sura hii iliposhuka Abubakar alikuwa amekaa, basi akaanza kulia. Mtume S.A.W akamuuliza "nikipi kinachokuliza ewe Abubakar? " Abubakar akajibu " ni hii sura " basi Mtume wa Allah akasema "lau kama nyinyi mngelikuwa si wenye hamkosei na hamfanyi madhambi basi Allah angeumbwa umma mwingine baada yenu ambao watu wake wanakosea na wanafanya madhambi na kisha wanataka msamaha na Allah atawasamehe"
KIPENGELE CHA TAWHID:
Sura hii ukiisoma kwa mazingatio Ina mambo mengi ya kiimani tunapasa kuyaweka katika fahami zetu:
1. Ardhi itatetemeshwa na itoe kila kilichomo ndani yake marehemu na hazina zilizomo
2. Mwanadamu atapata hofu sana na kujiuliza ina nini hii ardhi
3. Siku ya kiyama Ardhi itatoa siri zote, itatoa ushahidi wa kila wema na uovu uliofanywa na mtu katika ardhi.
4. Allah ameipa idhini Ardhi ianze kutoa habari. katika surat Yasin Allah anatujulisha kuwa siku ya kiyama midomo yetu haitafanya kazi, yaani haitazungumza, ila Allah atazungumzishwa viungo na viseme yaliyo ya kweli, viungo hivyo ni kama mikono, ngozi na vinginevyo. Hivyo hivyo ardhi nayo itapewa idhini ya kuzungumza kweli tupu kila kilichofanywa na mwanadamu iwe kidogo aka kikubwa.
5. basi mwenye kufanya wema ama uovu ulio mdogo kama dhara basi atalipwa kama ni wema kwa wema na kama ni uovu kwa adhabu. Neno dhara hili leo linatafsiriwa kwa maana ya atom. Atom ni chembe ndoogo sana ambayo huwezi kuiona kwa macho ya kawaida kwa udogo wake. Hii inamaanisha kuwa hata kama wema ni mdogo kiasi gani utalipwa na hata kama uovu ni mdogo kiasi gani pia utalipwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
yaliyomo: HUKUMU YA MIM SAKINA, NUN SAKINA, MADA, WAQFU, QALAQALA, TAFKHIM NA TARQIQ, USOMAJI WA QURAN
DARSA ZA TAJWID YALIYOMOSURA YA 01 .
Soma Zaidi...Quran na sayansi
3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran??
Soma Zaidi...Hoja juu ya kukubalika hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Utofauti wa Quran na hadithi Al Quds
Has utakwenda kujifunza utofauti was Hadithi Al Quds na Quran
Soma Zaidi...