image

Hoja juu ya kukubalika hadithi

Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

7.0. SUNNAH NA HADITH.

     7.1. Hoja juu ya Kukubalika Hadith.

“Anachokupeni Mtume chukuweni na anachokukatazeni nacho kiacheni.”  (59:7).

“Anayemtii Mtume ameshamtii Mwenyezi Mungu.” (4:80)

Rejea pia Qur’an (52:3-4).

 

  1. Hadith hazikufuata mpango kama ulivyo mpangilio wa Qur’an wakati wa kushuka, kupangwa, kuhifadhiwa na kuandikwa.

 

Udhaifu wa dai hili;

-  Kutoandikwa kwa Hadith kama ilivyoandikwa Qur’an sio hoja na sababu ya kutokubalika Hadith.

-  Mtume mwenyewe aliwakataza Maswahaba kuandika Hadith wakati wa uhai wake.

 

  1. Baada ya kufa Mtume (s.a.w), waislamu waligawanyika makundi tofauti yanayopingana, na hata kuweza kubuni maneno na kudai kuwa ni Hadith za Mtume (s.a.w). Je utajuaje Hadith zilizosahihi?

 

Udhaifu wa Hoja hii;

-  Kuna Wanachuoni wenye msimamo madhubuti waliobobea katika elimu ya Hadith na hawakujihusisha na migogoro yeyote iliyozuka.

 

-    Vigezo vya kisayansi kama Isnad, Riwaya na Matin vilitumika katika kuchambua  usahihi na udhaifu wa Hadith.

 

  1. Hadith zilikusanywa na kuandikwa muda mrefu baada ya kufa Mtume (s.a.w) na Maswahaba. Je kuna ushahidi gani unaothibitisha kuwa maneno yaliyosemwa ni ya mtume (s.a.w)?

 

Udhaifu wa Hoja hii;

-  Sunnah ya Mtume (s.a.w) ni maelezo juu ya maisha yake ambayo maswahaba walirithishana baada ya kutawafu (kufa) Mtume.

 

-   Ukusanyaji na uandishi wa Hadith ulifanyika kwa utaalamu wa kisayansi katika kubaini ukweli wa Hadith.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/25/Tuesday - 10:05:39 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1520


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Sababu nyengine zilopelekea kushushwa kwa suratul ikhlas
Soma Zaidi...

quran na sunnah
Soma Zaidi...

QURAN: TAJWID, FADHIKA ZA KUSOMA QURAN, FADHILA ZA KUSIKILIZA QURAN, FAIDA ZA SURAT FATIHA, YASIN, BAQARA, TABARAK
Soma Zaidi...

Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili kuleta Umoja na Ukombozi wa Waarabu:
(vii)Dai kuwa Muhammad (s. Soma Zaidi...

Hoja juu ya kukubalika hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat An-Nasr (idhaa jaa)
SURATUN-NASR Sura hii imeteremka wakati Mtume (s. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa Surat At-Takaathur
Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii surat At-Takaathur ilishuka Makka, na hizi ndio sababu za kushuka kwa sura hii Soma Zaidi...

Sifa za waumini katika quran
Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

DARSA ZA QURAN
Soma Zaidi...

Fadhila za surat al-fatiha na sababu za kushuka kwake
1. Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma surat al Imran
Post hii itakufundisha fadhila na faida za kusoma surat al Imran Soma Zaidi...