Post hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa surat at Tin (watin wazaitun).
Surat at Tin ni sura ya 95 katika mpangilio wa Quran kama ilivyoandikwa kwenye Mashaf. Sura hii ina aya 8 na imeshuka Makkah. Mtume s.a.w alikuwa akiisoma sura hii wakati anaposwali swala ya safari.
Amesimulia Ala Baraa bin Azib kuwa alikuwa Mtume s.a.w akisoma katika swala za safa katika moja ya rakaa mbili alikuwa akisoma surat at Tin (watin wazaytun)……
Sababu za kushuka kwake.
Hakuna nukuu hasa za kuonyesha kama kulikuwa na tukio maalumu lililopelekea kushuka sura hii. Kuna baadhi ya kauli ni kuwa kuna swahaba alimfuata Mtumr s.a.w navkumuuliza kuhusu watu ambao ni wazee, na wana matatizo ya kusahau, ama ya akili, vipi amali zao je wataendelea kulipwa? Hapo ndipo ikashuka sura hii.
Sura hii imrjibu vyema swali hilo. Allah anasema wale waliokuwa na imani na kufanya matendo mema basi wana wao malipo yasiokatika.
Maana ya tin, zaitun na mlima sinai
Wametofautiana wafasiri kuhusu maana ya tin na zaitun. Wapo waliosema kuwa hii ni misikiti, yaani msikiti wa Damaska na wa palestina Bayt al Maqsid.
Ila uhakika wa maneno na kaulicyenye nguvu makusudio hapa ni matunda mawili haya yani tunda Tini na tunda Zaituni. Matunda haya yanafahamika kwa kuwa navladha nzuri na manufaa makubwa kwa afya. Allah anaapia kwa kitu chochote kile akitakacho.
Makusudio ya mlima sinai, huu ni mlima ambao Nabii Musa alikuwa akizungunza na Allah. Na Mji wa amani uliotajwa makusudio ni Makkah ambapo kuna msikito mtukufu zaidi.
Ujumla wa sura hii
Sura hii Allah ameanza kuapa kisha akatupa masingatio kuwa hakika mwanadamu ameumbwa katika umbo zuri. Kisha akatupa mazingatio kuwa mwanadamu huyu aliyekuwa katika umbo zuri endapo atafanyavmatendo mema atabakia katika hadhi yake ya juu. Na endapo atamuasi Allah atushushwa awe na hadhi ya chini kabisa katika wenye hadhi za chini.
Allah akatupa mazingatio menginr kuwa wale wanaomuamini Allah ana kufanya matendo mema wana wao malipo yasiokatika.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Qalqala imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Qalqalatul qubra yaani qalqala kubwa na qalqalat as shughura yaani qalqala ndogo.
Soma Zaidi...SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah.
Soma Zaidi...Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr.
Soma Zaidi...Unazijua faida za kusoma Quran, na je ni faida gani utapata ukisoma Quran?
Soma Zaidi...Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w , sehemu ya 19. Hapa utajifunza maisha ya Mtume kabla ya utume.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukuorodheshea aina saba za viraka vya usomaji wa Quran.
Soma Zaidi...