Sura hii ni katika sura za kitawhidi sana. Maulamaa wanasema inatosha sura hii kuwa ni mawaidha. Imamu sharifu anasema kuwa sura hii inatosha kuwa muongozo…
SURAT AL-ARS
Wafasiri wengi wanasema sura hii ilishuka Makka.
Imam Shafii anasema, Sura hii ina maana nyingi na pana. Na kama mtu aifikiri, haja zake zote za dini zinaweza kutimizwa. Imesimuliwa katika Hadithi ya kuwa masahaba wawili kila mara walipokuwa wanakutana wakati wa kuagana walikuwa wakisomeana sura hii.
Neno hili maana yake ni wakati, wakati wa alasiri, na pia maana yake ni kukamua. Katika Aya hii Mwenyezi Mungu analeta ushahidi wa wakati kuonyesha ya kwamba kadiri wakati unavyopita umri wa kila mtu unapungua na kuingia katika hasara maana kila kitu kinasogelea mwisho wake na kitakufa. Lakini watu wanaweza kujiepusha na hasara hiyo kwa kuamini na kutenda mema na kuusiana kushika haki na subira, maana mambo haya yatafanya roho zao ziendelee katika maisha ya raha huko Akhera.
Katika sura hii habari za watu wa namna mbili zimeelezwa. Ya kwanza ni wale ambao wamo hasarani, na pili ni wale ambao wameamini na kufanya vitendo vizuri. Ni dhahiri ya kuwa wasioamini wala hawafanyi vitendo vizuri wao ndio watakaokuwa katika hasara. Lakini wanaoamini kwa moyo wote, tena wanaionyesha imani yao kwa viungo vyao, kwa kutenda sawa na walivyoamini, bila shaka wao watalindwa na hasara. Tena ikumbukwe ya kuwa Mwenyezi Mungu aliposema "walioamini" kwa hakika ameashiria kwenye ukamilifu wa elimu; maana imani haiwezi kupatikana bila elimu, Basi mtu anapopata ukamilifu katika elimu, anakuwa mwenye imani hasa. Na Mwenyezi Mungu aliposema "kufanya vitendo vizuri" ameelekeza kwenye ukamilifu wa amali, yaani matendo. Hivyo Mwenyezi Mungu amesema ya kuwa watu wanaokamilika katika elimu, na wanaokamilika katika vitendo, wao wanasalimika katika hasara na wanaokoka.
Hakuna sababu maalumu yenye kuaminika juu ya kushuka kwa sura hii.
UMUHIMU WA SURA HII
Sura hii inachukuliwa kama muhtasari wa Qur'ani nzima na karibu wasomi wote mashuhuri wa kitamaduni na wa kisasa wa Kiislam wakiwemo Imam Shafi, Ibn Kathir, Israr Ahmed na Farhat Hashmi.
Ibn Kathir, mfasiri wa Quran anashikilia kwamba sura hii, kama onyo kwa waumini kutopoteza wakati au wangeweza kudhalilishwa au hata kuharibiwa.
Imam Shafi, alishikilia-kwamba ikiwa Mungu angefunua tu surah hii ingetosha kwa mwongozo wa wanadamu wote. Ilielezea kwa muhtasari kiini cha ujumbe wa Kurani. Kwa hivyo, Imam Shafi'i anasisitiza kwamba ikiwa mtu angefuata ushauri wake, ilitosha kwa wanadamu kupata mafanikio maishani.
Sayyid Qutb, Mfasiri wa Quran, anathibitisha kwamba surah hii inaelezea mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu kulingana na maoni ya Kiisilamu. Anasema kuwa inafafanua, kwa njia iliyo wazi na fupi zaidi, dhana ya kimsingi ya imani katika muktadha wa ukweli wake kamili.
Al-Tabarani: wakati wanadamu wanajikuta wamepotea; inaweza kujihuisha kwa kurudi kwenye fomula iliyotolewa na aya ya tatu na kanuni / masharti manne, ambayo yanazingatiwa kama msingi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA : Mym sakina ni miym ambayo haina iβrab ( Ω Ω).
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha fadhila na faida za kusoma surat al Imran
Soma Zaidi...Qur-an inavyogawa MirathiMgawanyo wa mirathi umebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili.
Soma Zaidi...Kusoma Qur'an kuna faida kubwa kwa Muislamu, kwanza kunampatia thawabu, kunatoa nuru maisha yake, mwili wake na kumlinda na mashetani na watu wabaya. Quran ni dawa na pozo kwa magonjwa. Thawabu za Qur-an hulipwa kwa kila herufi. Quran pia huja kutet
Soma Zaidi...3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran??
Soma Zaidi...(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid
Soma Zaidi...