image

Sababu za kushuka kwa surat Al-Humazah

Zijuwe sababu kuu za kushuka surat Al-Humazah katika quran

<<<<<<< HEAD Sababu za kushuka kwa surat Al-Humazah

Surat Al-Humazah

SURAT ALHUMAZAH
Sura hii imeteremshwa Maka na ina aya 10 pamoja na bismillah.
Wafasiri wengi wanakubaliana ya kuwa sura hii ilishuka Makka. Hali ya watu wa siku za Mtume s.a.w. waliokuwa wakiwaudhi Waislamu na wakijivuna kwa mali zao, imeelezwa katika sura hii.Humazah, "Msingiziaji." Neno hili limetoka katika neno hamazah lenye maana ya
kusingizia; kukoneka; kupiga kwa kidole; kusukumu; kupiga; kuuma; kusengenya; kuvunja; kutia wasiwasi.Lumazah (Msingiziaji) ni neno lililotoka katika lamazah, yaani kusingizia, kuaibisha; na ku- koneka.Masahaba na watu wa baadaye wamehitilafiana katika maana ya Aya hii, na hakuna sababu yake nyingine isipokuwa ya kwamba maneno haya mawili humazah na lumazah yanakaribiana sana katika maana. Inasemekana ya kuwa Mughira, A'as bin Wail na Sharik walikuwa wakishughulika kila mara kumwudhi Mtume s.a.w. na masahaba kwa kuwasingizia na kuwaaibisha; basi Mwenyezi Mungu katika sura hii akawaonya ya kuwa waache mwendo wao huo waila wataangamizwa.Lakini hakuna haki ya kusema ya kuwa watu hawa watatu tu ndio walioonywa, maana
wangekuwa ni hao watatu tu, basi wangetajwa majina yao. Lakini badala ya kutajwa majina yao Mwenyezi Mungu amesema, Maangamizo kwa kila msingiziaji, msengenyaji. Hili laonyesha ya kuwa watu wote wenye ada na mwendo wa namna hiyo wameonywa - wawe watu wa zamani, wa leo, hata na wa baadaye - wote watapata adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zao za kuwasingizia, kuwaaibisha, kuwasengenya na kuwateta watu. Hivyo, Mwenyezi Mungu amewaonya
watu wote wa siku zote ili wasishike njia ya namna hii inayoleta machafuko makubwa kati ya jamii za watu na makabila, na watu wanatenguka nguvu zao na kuangamia kabisa.
                   ======= Sababu za kushuka kwa surat Al-Humazah

                   >>>>>>> origin/master           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 251

Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Sababu za kushuka kwa Surat al-Kawthar na fadhila zake
SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail. Soma Zaidi...

Maana ya Quran na Majina ya quran n amaana zao
Soma Zaidi...

Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili Kuwania Madaraka na Ukubwa
(x) Dai kuwa Muhammad (s. Soma Zaidi...

Tafsiri na mafunzo ya sura zilizochaguliwa - Saratul-fiyl
Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa Surat At-Takaathur
Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii surat At-Takaathur ilishuka Makka, na hizi ndio sababu za kushuka kwa sura hii Soma Zaidi...

Maudhui ya Qur-an na Mvuto wa Ujumbe Wake
Soma Zaidi...

Quran si maneno ya mwenye kifafa
Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

Sababu nyengine zilopelekea kushushwa kwa suratul ikhlas
Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma surat al Fatiha (Alhamdu)
Post hii inakwenda kufundisha fadhila na faida za kusoma Alhamdu. Soma Zaidi...

quran na sunnah
Soma Zaidi...

HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...