Sura hii iliposhuka ilikuwa kama imekuja kuwasuta Wanafiki waliokuwa wakizungumzahabari za uongo kuhusu jeshi alilolituma Mtume wa Allah.
Ibni Mas'ud, Jabir, Al-Hasan, Ikrama na Ataa wanasema ya kuwa sura hii ilishuka Makka.
Dhabhan ni namna moja ya mbio za wanyama (Mufradat); tena ni sauti maalumu inayotoka katika vifua vya farasi wanapokimbia (Akrab). Wakimbiaji wanaotweta, mradi wa maneno haya ni farasi.
Abdullah bin Abbas na wanazuoni wengine kama Mujahid, Ikrama, Ataa, Qatada na Dhahhaak wote wanakubali ya kuwa mradi ni farasi. Na lugha ya Kiarabu pia inasaidia maana hii.
Iliposhuka sura hii watu walikuwa na ngamia, na hakukuwa sana desturi ya kuwatumia farasi. Lakini Mwenyezi Mungu kwa kuiteremsha Aya "Wakimbiaji wanaotweta" akabashiri ya kuwa hawa watu wa Makka wapandao ngamia siku moja watakuwa wapandao farasi.
Na kweli, baadaye desturi ya kuwapanda farasi ilienea sana, na farasi wakazidi kabisa, na Waislamu wakawa wakimbiaji juu ya farasi katika matukio ya vita na amani.
Kwa neno zima, Aya hii inajulisha ya kuwa Waislamu walikuwa na shauku na huba sana ya kuitumikia dini, hata wakawabana maadui waliokuwa na nguvu nyingi na silaha kubwa. Wao walikuwa wanakwenda mbio na wakiwakimbiza farasi kwa kutoa sadaka maisha yao.
Sababu za kushuka sura hii:
Muqatil amesema kuwa Mtume s.a. w Alituma jeshi liende kabila la bani Kinana na akamteua Mundhir bin Amr al Ansariy awe kama kiongozi wa jeshi hilo.
Sasa muda mrefu umepita yapata mwezi habari za jeshi hili hazikufika Madina. Wanafiki wakaanza kutangaza kuwa wotevwaneuliwa.
Hapo ndipo Allah akatoa taarifa za jeshi hili na kisha ikashuka sura hii.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Hukumu za kim sakina na tanwin ni idgham shafawiy, idh-har shafawiy, na Ikhfau shafawiy
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane.
Soma Zaidi...(i)Mtume Muhammad (s.
Soma Zaidi...ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.
Soma Zaidi...