Posti hii inahusu zaidi namna chanjo ya polio inavyotolewa na ratiba zake yaani kuanzia siku ya kwanza mpaka pale mtoto anapomaliza chanjo hii kwa hiyo tuone ratiba ya chanjo ya polio.
Ratiba ya chanjo ya polio.
1.Kwanza kabisa tunajua kuwa hii chanjo utolewa kwa watoto wadogo kwa vipindi mbalimbali kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya, chanjo hii utolewa kwa watoto tu na njia inayotumika ni kupitia kinywani kwa njia ya matone kwa hiyo chanjo hii utolewa kwa vipindi maalumu kama ifuatavyo.
2.Kipindi cha kwanza ni pale mtoto anapozaliwa anapaswa kupata chanjo hii kwa njia ya matone mawili kupitia mdomoni ,chanjo hii huwa katika vichupa viwili kichupa cha kwanza huwa na Poda na kichupa cha pili kina maji ya kuchanganya na chupa hizi mbili zinapaswa kutoka kwenye kiwanda kimoja kama ni viwanda tofauti upaswi kuzitumia.
3.Chanjo ya pili Mtoto ana paswa kupewa baada ya wiki sita ambapo ni sawa na mwezi mmoja na wiki mbili kwa hiyo mama anapaswa kubwa siku ya kumrudisha mtoto kupata chanjo na kwenye hili udhurio Mtoto ataendelea kupata matone mawili kama kawaida na baadae ndio yataweza kubadilika.
4.Chanjo ya tatu mtoto anapaswa kuipata baada ya wiki kumi ambazo ni sawa sawa na miezi miwili na wiki mbili kwa hiyo mama anapaswa kuandikiwa nyuma ya kadi yake siku ya kumrudisha mtoto ili apatiwe chanjo kwa hiyo Mama ataleta mtoto waka na kwa mda huu atapata matone mawili mdomoni na atarudi kwenye wiki ya Kumi na nne kwa ajili ya kumalizia chanjo.
5.Chanjo ya nne mtoto akarudishwa kwenye wiki ya Kumi na nne ambayo ni sawa na miezi mitatu na wiki mbili mtoto atapewa chanjo kwenye paja la la Kushoto kiasi cha moja nukta tano millis kwenye mguu wa kushoto , kwa hiyo mtoto akichukua chanzo zote anakuwa amekamilisha chanjo na ni vigumu kupata Ugonjwa wa kupooza .
6.Kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua umuhimu wa chanjo ya polio ili kuweza kuokoa maisha ya watoto na kwa wale wanaokuwa wazembe kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo wanapaswa kuchukuliwa hatua ili waweze kuokoa maisha ya watoto na kuondokana na kuwatunza watu wenye ulemavu na kupunguza pato la taifa kwa hiyo tunapaswa kuwa makini na kuhakikisha kubwa watoto wanapata chanjo ya polio na elimu itolewe kwenye jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo utolewa kwa watu wanaodhani wamepatwa na maambukizi ya virus vya ukimwi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu njia za kumlisha Mgonjwa ambaye hawezi kujilisha wenyewe, hali hii uwa inawapata wagonjwa wale ambao hawawezi kujilisha wenyewe tunaweza kuwalisha kwa njia zifuatazo.
Soma Zaidi...Hata kama mtu atakuambbia usile vyakula yenye mafuta bado itahitajika kula tu. Kuna mafuta na fati je unajuwa utofauti wao. Ni zipi kazi zao mwilini? Endelea na makala hii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuondoa sumu mwilini, ni njia mbalimbali ambazo uweza kutumika ili kuondoa sumu mwilini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli.
Soma Zaidi...Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na minyoo
Soma Zaidi...Poshi hii inahusu madhara ya ulevi.Utegemezi wa pombe kwa kawaida humaanisha kuwa mtu anatumia kiasi kikubwa cha pombe na kuna masuala kuhusu kupoteza udhibiti.
Soma Zaidi...Post hii inahusu namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyeungua moto, kuingia moto ni kitendo Cha kubabuka ngozi ya juu inaweza kuwa kwa kemikali,umeme na just,
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyezimia
Soma Zaidi...