imageimage TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN
Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao.
TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURANI
Mtume ameamrisha watu waihifadhi qurani. na sihivyo tuu Mtu aliyehifadhi qurani ajitahidi anafanya jitihada isije akaisahau. Katika hadithi sahihi Mtume anazungumzia kuwa qurani itakimbia kama inavyokimbia kamba ya ngamia.

Kusahau qurani baada ya kuihifadhi ni katika madhambi. Hivyo wasomaji wa qurani tujitahidini kuihifadhi na kuhakikisha pale tulipopahifadhi tunapashikilia pasiondoke. Amesimulia Anas ibn Maliki kuwa Mtume amesema “nilioneshwa malipo ya uma wangu (nikaona kuna malipo ) mpaka kwenye uchafu anaouondoa mtu msikitini. Na nilioneshwa madhambi ya uma wangu, basi sikuona dhambi kubwa kuliko sura katika qurani au aya aliyopewa mtu kisha akaisahau” (amepokea Abuu Dauw, Tirmidh na Ibn Majah).