Sababu za kushuka surat al qadir

Asbab nuzul surat al qadi. Hii ni sura ya 97 katika mpangilio wa mashaf. Surat al qadir imeteremshwa Madina na ina aya 5.

Kwa kauli ya Jamhuri sura hii imeshuka Madina. Zipo baadhi ya kauli kuwa ni ya Madina. 

 

وَذَكَرَ الْوَاقِدَيُّ أَنَّهَا أَوَّلُ سُورَةٍ نَزَلَتْ بِالْمَدِينَةِ. وَهِيَ خَمْسُ آيَاتٍ.

Na katika kauli nyingine ni kuwa hii ndio sura ya kwanza kushuka Madina. Angalia tafsir al qurtub. 

 

Asbab nuzuli - sababu zakushuka

عَنْ مُجَاهِدٍ قَالَ : ذَكَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَبِسَ السِّلَاحَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَلْفَ شَهْرٍ ، فَتَعَجَّبَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ ذَلِكَ ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى : ﴿إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ [1] وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ [2] لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ﴾ . قَالَ : " خَيْرٌ مِنَ الَّتِي لَبِسَ فِيهَا السِّلَاحَ ذَلِكَ الرَّجُلُ " .

Amesema Mujahid kuwa Mtume s.a.w alimtaja Mtu mmoja katika wana wa Israel kuwa alivaa silaha za vita kwa ajili ya njia ya Allah (kupigana jihadi) kwa muda wa miaka elfu moja. Basi Waislamu (Masahaba) walistaajabu sana na habari hii basi hapo Allah akishika sura hii ﴿إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ [1] وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ [2] لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ 

 

Akasema Mtume "Ni bora kuliko yule mtu aliyevaa vazivla vita (kwa miaka elfu). 

 

Usiku wa laylat al qadir

Usiku wa heshima. Katika sura 2:186 imesemwa ya kuwa Qur'an ilishuka katika mwezi wa Ramadhani. na katika sura hii inasemwa ya kuwa iliposhuka ilishuka katika usiku  unaoitwa Lailat al-Qadir, yaani usiku wenye heshima. Sio mradi wake kuwa Qur'an yote ilishuka  katika mwezi mmoja au usiku ule mmoja, bali mwanzo wa kushuka ilikuwa ni katika usiku wa Qadr wa mwezi wa Ramadhani na ikaendelea kushuka kwa miaka 23.

 

Siku moja Mtume aliambiwa na Mwenyezi Mungu usiku huu ni tarehe gani ya mwezi wa 
Ramadhani. Alipokuwa akitoka ili kuwapa watu habari akakuta watu wanagombana na akaingia 
kuwaamua. Katika kuamua, tarehe ile akaisahau, lakini akasema watu wanaweza kuitafuta Lailat 
al-Qadr katika tarehe 21 au 23 au 25 au 27 au 29 ya mwezi wa Ramadhani (Bukhari). Lailat 
al-Qadir huendelea mpaka alfajiri, ndiyo mwisho

Soma zaidi kuhusu usiku huu Bofya hapa

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 2198

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Sababu za kushuka Surat al Kafirun

Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.

Soma Zaidi...
Nini maana ya Quran

Post hii inakwenda kukuambia maana ya Quran

Soma Zaidi...
Ni nini maana ya id-gham katika hukumu za tajwid

Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake.

Soma Zaidi...
quran tahadhari

TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al-Fiyl

Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat Ikhlas

Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani?

Soma Zaidi...
Fadhila za kusoma surat al Imran

Post hii itakufundisha fadhila na faida za kusoma surat al Imran

Soma Zaidi...