(iv)Qur-an Kushuka Kidogo Kidogo kwa Kipindi cha Miaka 23:
Historia inatuthibitishia kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) hakuanza kuufundisha Uislamu na kuutangaza ulimwengu mzima kwa kurejea Qur-an kama Kitabu tulicho nacho hivi sasa bali aya za Qur-an zilikuwa zikimshukia kidogo kidogo kulingana na haja na wakati kwa kipindi chote cha Utume wake cha miaka 23. Kwa maana nyingine Qur-an imeshuka kidogo kidogo katika kipindi chote cha utume kuanzia mwanzo wa Utume 610 A.D. mpaka siku chache kabla ya kutawafu Mtume(saw), 632 A.D. Kuhusu Qur-an kushuka kidogo kidogo tunafahamishwa katika aya zifuatazo:
Na Qur-an tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogo kidogo. (17:106)
Na wakasema wale waliokufuru; Mbona hakuteremshiwa Qur-an yote kwa mara moja? Kama hivi (mnavyoona, tumeiteremsha kidogo kidogo) ili tuuthibitishe, (tuutie nguvu), moyo wako (kwa hizo aya mpya mpya zinazoteremshwa wakati baada ya wakati) na tumeipanga kwa uzuri. (25:32)
Hakika sisi tumekuteremshia Qur-an sehemu sehemu (kidogo kidogo). (76:23).
Kama inavyoonekana katika aya hizi. Qur-an imeshushwa kidogo kidogo ili iwe wepesi kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kuufikisha ujumbe uliotangulia kwa ukamilifu kinadharia na kimatendo kabla ya ujumbe mwingine uliofuata.
Kwa upande mwingine Qur-an imeshuka kidogo kidogo ili kuwawezesha waumini wa mwanzo kuihifadhi Qur-an kwa wepesi, kuyaelewa fika mafundisho yake kinadharia na kuwawezesha kuitekeleza Qur-an katika kila kipengele cha maisha yao ili wawe jamii bora ya kuigwa na jamii zitakazofuatia.
Kushuka Qur-an kidogo kidogo kwa muda wa miaka 23 ni hoja nyingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w). Kwa yeyote yule anayeisoma Qur-an kwa makini na akajua mpangilio wake wa aya na sura kama vile sura moja kuwa na mchanganyiko wa aya za mwanzo na zilizoshushwa mwishoni lakini bado kunapatikana mtiririko mzuri wa maudhui na mpangilio wa sura usiofuata mtiririko wa kushuka, utaona kuwa haiyumkiniki kuwa Qur-an ni Kitabu kilichoandikwa na Mtume Muhammad (s.a.w) kama wanavyodai makafiri.
Pia Qur-an ingelikuwa imeandikwa na Mtume Muhammad (s.a.w) isingelichukua muda wote huo, bali ingelibidi aiandike yote kwa muda mfupi ili aweze kuitumia katika kazi yake ya kuwaongoza watu. Ni kawaida kuwa ili kufanikiwa katika utekelezaji wa jambo lolote ni lazima kwanza pawe na nadharia nzuri inayoelekeza namna ya utekelezaji. Halikadhalika, Mtume Muhammad (s.a.w) aliyekuwa kiongozi wa Dola ambaye mfano wake haujapatikana, asingeliweza kufanya kazi nzito na kubwa kiasi hicho bila ya kuwa na nadharia ya kumwongoza. Hivyo, kwa kutokuwa na Qur-an yote mkononi mwake ili kuitumia katika kila hatua ya kazi yake, inadhihirisha kuwa alikuwa akiletewa mwongozo kutoka kwa Allah(sw) katika kila hatua ya kazi yake mpaka alipoikamilisha.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1476
Sponsored links
👉1
Kitabu cha Afya
👉2
kitabu cha Simulizi
👉3
Simulizi za Hadithi Audio
👉4
Madrasa kiganjani
👉5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6
Kitau cha Fiqh
HIKUMU YA BASMALLAH YAANI KUSOMA BISMILLAH
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...
Quran haikutoka kwa Mtu zezeta wala mwenye upungufu wa akili
Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat Ikhlas
Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani? Soma Zaidi...
Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w)
Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s. Soma Zaidi...
HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...
Naman ya kuiendea quran na kuifanyia kazi baada ya kuisoma
Soma Zaidi...
quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...
Saratul-humaza
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Ni nini maana ya Tajwid, na ni ipi nafasi yake kwenye uislamu
Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid. Soma Zaidi...