(iv)Dai kuwa Qur-an ni zao la Mwenye Kifafa na Aliyepagawa na Shetani:
Waandishi kadhaa wa kikafiri katika maandishi yao wamedai bila kutoa ushahidi wowote unaotokana na historia kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa mwenye kifafa na mwenye kupagawa na Shetani na maneno yake alipokuwa katika hali ya ugonjwa ndiyo yaliyonukuliwa na kuunda Kitabu cha Qur-an!
Udhaifu:
Udhaifu wa dai hili tunaweza kuuona kwa kujiuliza maswali yafuatayo: Je, kifafa, ugonjwa mbaya kama tunavyoufahamu, umewahi kumtokea mtu katika historia ya mwanaadamu na bado akawa mtu mwenye kutoa sheria za kufuatwa na umati wa watu wengi zaidi ya robo ya dunia? Je, historia ya mwanaadamu imewahi kumshuhudia mgonjwa wa kifafa au mwenye kupagawa na shetani kuwa na hadhi na uwezo mkubwa kuliko mtu yeyote ulimwenguni kama ilivyokuwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w)? Kama mgonjwa wa kifafa ndiye aliyeandika Qur-an, inakuwaje waandishi hodari wenye akili timamu na wanafalsafa wakubwa washindwe kuandika kitabu mithili ya angalau sura moja ya Qur-an na kukabili changa moto iliyotolewa na Qur-an karne nyingi zilizopita:
"Je! Ndiyo wanasema ameitunga? Sema: "Hebu (tungeni na nyie) mlete sura moja mfano wake na waiteni muwezao (kuwapata waje).- isipokuwa Mwenyezi Mungu - (wa kuwasaidieni) kama nyinyi mnasema kweli (kuwa haya ameyazua Muhammad)." (10:38)
Kitaalam inafahamika kuwa ugonjwa wa kifafa baada ya muda humfanya mgonjwa kuwa taahira (punguani). Pia ugonjwa wa kifafa humdhoofisha mgonjwa na hutisha wauguzaji na wenye kumuangalia mgonjwa wakati ameshikwa na kifafa. Hapana ushahidi wowote katika historia ya Mtume (s.a.w) ambayo iko bayana mno kuliko historia ya mtu yeyote, kuwa alikuwa mwenye kifafa au mwenye kupagawa na shetani.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr.
Soma Zaidi...SURATUL-KAFIRUN Imeteremshwa maka na inaelezwa katika sababu za kushuka kwake ni kuwa Kundi la makafiri lilimfuata mtume (s.
Soma Zaidi...Sura hii ni miongoni mwa Sura fupi sanya huwenda ndiosura yenye aya chache kuliko sura zote katika Quran.
Soma Zaidi...surat Zalzalah ni sura ya 99 katika mpangilio wa Quran, na ina aya 8. Sura hii imeteremshwa Madina ila pia kuna kauli zinathibitisha kuwa ni ya Makkah. Katika hadithi iliyopewa daraja la hassan na Imam Tirmidh Mtume S.A.W amesema kuwa kusoa surat Zilzalah
Soma Zaidi...MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.
Soma Zaidi...