Menu



As-Sab nuzul

Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran.

As-Sab nuzul

Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura
Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran. Basi ijulikane kuwa Quran imeshuka kwa muda wa miaka 23 kidogo kidogo. Na ilikuwa mara nyingi ikishuka linapotokea tukio. Hivyo Allah alikuwa akiishusha qurani kuwa kama muongozo kwa lililotokea.

1.SURAT AL-FATIHA.
Muhadithina wengi wanaeleza ya kuwa sura hii nzima ilishuka Makka, na toka mwanzo ilikuwa ni sehemu ya maombi ya Waislamu. Hii ndiyo sura iliyotajwa katika aya ya Qur'an, Na kwa yakini Tumekwisha kupa (Aya) saba zisomwazo mara kwa mara na Qur'an kubwa (sura 15:88), ambayo ilishuka Makka. Habari zingine zinaeleza ya kuwa sura hii iliteremshwa tena mara ya pili, Madina. Sura hii ilishuka mapema tu Mtume s.a.w. alipoanza kazi.

MAJINA YA SURA HII NA MAANA YAO.
Jina maarufu la sura hii ni Faatihat-ul-Kitaab (Inayofungua Kitabu) (Tirmidhi na Muslim). Baadaye jina hilo lilifupishwa kuwa Surat-ul-Faatihah, au Al-Faatiha. Sura hii imepewa majina mengi, na haya kumi ndiyo yaliyo sahihi zaidi: Al-Faatiha, As-Salaat (Sala), Al-Hamdu (Sifa njema), Ummul-Qur'aan (Mama ya Qur'an), Al-Qur'aan-ul-Adhiim (Qur'an Kubwa) As-Sab'ul-Mathaani (Aya saba zinazosomwa mara kwa mara), Ummul-Kitaab (Mama ya Kitabu), Ash-Shifaa (Ponyo), Ar-Ruqya (Kago), Al-Kanz (Hazina).

Maulamaa wa elimu za Qurani hawakutoa zaidi ufafanuzi wa sababu ya kushuka kwa sura hii. Au jambo hili halikuwashughulisha kabisa.

2.SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS)
Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s.a.w) alirogwa na wachawi wa kiyahudi kwa kutumia nywele zake kisha uchawi ule wakautumbukiza kwenye kisima cah Banu quraidha, na aliyewapa nywele wachawi hao ni labid ibn Aā€™swam. Mtume aliumwa kwa muda wa miezi sita iala uchawi huu haukuathiri akili yake. Hata sikumoja alipolala wakaja malaika wawili na mmoja wao akaulia kumuuliza mwenziwe ā€œana nini huyu (Mtume)ā€¯ yule wa pili akajibu ā€œamerogwaā€¯ kisha akaeleza namna alivyorogwa na mwisho akkaeleza tiba ya uchawi ule ndipo akasoma sura mbili hizi. Na hii ndiyo husemwa sababu ya kushuka kwa sura hizi. Sura hizi zimeteremka madina.

3.SURATUL-IKHLAS.
Inaelezwa kuwa walimfuata Mayahudu kumfata mtume (s.a.w) na kumwambia awasifie namna ambavyo Mola wake alivyo ndipo Allah akaishusha sura hii. Pia katika kauli nyingine ni kuwa Makafiri waliokuwa wakiabudia masanamu walimwendea Mtume (s.a.w) na kumwambia awaeleze sifa na namana Mola wake alivyo ndipo Allah akateremsha sura hii. Sura hii ni katika sura za mwanzo kabisa kushuka Makka na mafundisho yake yanavunja kabisa ibada ya masanamu na Ukristo na kila mafundisho ya miungu wengi.

Mama Aisha anasimulia ya kwamba Mtume s.a.w. alipokuwa akienda kitandani kwake kila usiku, aliunganisha vitanga vya mikono yake, kisha anavisomea Qul huwallaahu na Qul a'uudhu birabbil falaq na Qul a'uudhu birabbinnaas, na anavipulizia, kisha anavipaka mwili wake wote kila anapoweza kupagusa toka kichwani; na akifanya hivyo mara tatu (Bukhari jalada la 3).

4.SURATUL-MASAD
Sura hii pia ni katika sura za kushuka Maka. Wanaeleza Maulamaa kuwa sababu ya kushuka sura hii ni kuwa mtume (s.a.w) alipopewa amri ya kulingania bila ya siri aliwaita watu wa Maka ili awalinganie na hapo baba yake mdogo Mtume (s.a.w) aitwaye Abdul ā€œUzza ambaye Qurani imemuita Abuu Lahabi yaani baba wa moto alitowa maneno ya upumbavyu na upuuzi juu ya ujumbe wa Allah na hapo Allah akateremksha sura hii.

Huyu Abu Lahab jina lake hasa ni Abdul Uzza, naye alikuwa baba mdogo wa Mtume s.a.w. Neno Abuu Lahab - baba wa miali ya moto - ni jina ambalo hutumika kwa ajili ya mtu ambaye hali yake n nya asili ni ya moto na ya uasi, na pia hutumika kwa ajili ya mtu ambaye anawachochea wengine. Hivyo bwana huyu amepangwa jina hili na Qur'an kwa sababu ya uadui wake kwa Mtume s.a.w. Siku ya kwanza Mtume alipowaita Wakureishi ili kuwaeleza habari za ujumbe wake, huyu Abu Lahab, alimkaripia akasema, "Uangamizwe, je umetuitia maneno haya!" (Bukhari). Na ilikuwa desturi yake kila mara kumfuata Mtume aendako na kuwaambia watu wasimsikilize, akisema, Mtume ni jamaa yake na ni mwehu. Kadhalika mkewe Abu Lahab aliyeitwa Ummi Jamil bint Harb, dada wa Abu Sufiyan, alikuwa mwanamke mbaya sana aliyekuwa anamwudhi sana Mtume na kumsumbua na hata kumsingizia-singizia mambo ya upuuzi. Na kwa sababu ya masingizio yake ameitwa mchukuzi wa kuni (Bukhari), ambazo kwazo amejikokea moto wa Jahanamu, (Razi).

SURATUN-NASR
Sura hii inaitwa ya Madina kwa kuwa ilishuka baada ya Mtume kuhama ingawa iliposhuka ilikuwa ni katika Makka wakati Mtume alipokwenda kufanya Haji ya mwisho. Na Ushindi mkubwa uliotajwa hapa ni ushindi wa Makka ilipoingia katika mamlaka ya Waislamu, mwaka wa 8 wa Hijra, na mwaka uliofuata ikawa makundi-makundi ya makabila ya Waarabu yanakuja ingia Uislamu. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotimiza bishara Zake za ajabu; na Mtume s.a.w. anaambiwa aombe ghofira kwa ajili ya makundi hayo yatakayoingia Uislamu maana kazi ya kusimamisha sheria ilikuwa kubwa. Seyidna Abu Bakar iliposhuka sura hii alilia. Watu wakamwuliza mbona unalia? Akajibu, Kazi ya Mtume s.a.w. sasa imekwisha na Atatutoka.

SURATUL-KAFIRUN
Imeteremshwa maka na inaelezwa katika sababu za kushuka kwake ni kuwa Kundi la makafiri lilimfuata mtume (s.a.w) na kutoa rai ya kuwa Mtume (s.a.w) ajiunge nao na aabudu miungu yao kwa muda wa mwaka mmoja na wao wataabudu Mola wake kwa muda wa mwaka mmoja. Na kisha ikionekana dini ya mtume (s.a.w) ni bora zaidi wataifuata na kama yao itakuwa ni bora zaidi ataifuata. Allah akalipinga jambo hili na akateremsha sura hii.


                   

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 699


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Aina za Madda twabiy kwenye usomaji wa Quran
Madda zimegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni madda twabiy na madda fariy Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa Surat Al-Asr
Surat Al-Asri imeteremshwa Makka, na hapa utazujuwa sababu za kushuka kwa sura hii Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma surat al Baqarah
Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii. Soma Zaidi...

Adabu za kusikiliza quran
ADABU ZA KUSIKILIZA QURANI 1. Soma Zaidi...

Uthibitisho kuwa quran ni maneno ya Allah kutokana na Historia (Hadith)
Soma Zaidi...

Aina za usomaji wa Quran
Je kuna aina ngapi zabusomaji wa Quran Soma Zaidi...

Sababu za kushukasurat an Nasr
Sura hii ni katika sura za mwisho kushuka, huwendakuwa ndio ya mwisho kabisa. Masahaba waliamini kuwa sura hii imetabiri kifo cha Mtume S.A.W Soma Zaidi...

Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w)
Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s. Soma Zaidi...

Kutokea Kweli Matukio yaliyotabiriwa katika Qur-an
Soma Zaidi...

MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...