Uthibitisho kuwa quran ni maneno ya Allah kutokana na Historia (Hadith)
(b)Uthibitisho kutokana na Historia (Hadith)
Historia ya kushuka Qur-an na namna Mtume (s.a.w) alivyoipokea ni ushahidi mwingine unaotuthibitishia kuwa Qur-an si kitabu alichokitunga Muhammad (s.a.w). Kuna maelezo kadhaa ya kihistoria tunayojifunza katika Hadith juu ya namna Mtume (s.a.w) alivyoipokea Qur-an. Hebu turejee hadithi zifuatazo:
(1)Hadithi ya bibi Aysha (r.a) iliyopokelewa na Imamu Bukhari inatufahamisha namna Mtume (s.a.w) alivyopokea wahyi wa kwanza wa Qur-an alipokuwa katika pango la Jabal Hira. Kama tulivyojifunza katika hadithi hiyo Mtume (s.a.w) alistushwa sana na tukio lile la kujiwa na Malaika Jibril (a.s) na kumuamrisha kusoma kinyume na uwezo wake. Tukio lile lilimhofisha sana Mtume (s.a.w) na kumfanya arejee nyumbani kwake akiwa anatetemeka. Tukio la Jabal Hira ni ushahidi mwingine tosha kuwa Qur-an si maneno ya Muhammad (s.a.w) bali ni ujumbe kutoka kwa Allah (s.w) uliofikishwa kwake kwa njia ya wahyi kupitia kwa Malaika Jibril.
(2)Mtume (s.a.w) alikuwa akibadilika haiba yake na kutokwa na jasho wakati wa kupokea wahyi kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
Bibi aysha (r.a) amesimulia: Kwa hakika nimemuona Mtume akiteremshiwa wahyi siku ya baridi kali na baada ya kumaliza kile kipindi cha kuteremshiwa wahyi alimininikwa na jasho jingi kichwani mwake." (Malik)
Amesimulia Aysha (r.a), "Al-Harith bin Hisham (r.a) alimuuliza Mtume wa Allah, 'Ee mtume wa Allah! Ni vipi wahyi unakuja?' Mtume wa Allah alijibu, "Wakati mwingine ulifunuliwa kwangu kwa sauti mithili ya mlio wa kengele, wahyi ulioletwa kwa namna hii ulikuwa mgumu sana kuliko aina nyingine zote (za wahyi), kisha hali hii ilikwisha baada ya kukidhibiti kile kilichofunuliwa. Wakati mwingine Malaika
(Jibril) alikuja katika umbile la binaadamu na kuzungumza nami, ambapo nilikidhibiti (nilikichukua) chochote kile alichosema." Aysha (r.a) aliendelea kusema: Hakika nilimuona Mtume (s.a.w) wakati anateremshiwa wahyi siku ya baridi kali na kuona jasho likitiririka usoni mwake." (Bukhari)
Hadithi hizi nazo zinatuthibitishia kuwa Qur-an si utunzi wa Muhammad (s.a.w) kabisa,bali ni ujumbe wa Allah (s.w) uliopitia kwake kwa njia ya wahy.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
As-Sab nuzul
Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran.
Soma Zaidi...Maisha ya Mtume Muhammad s.a.w kabla ya utume
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w , sehemu ya 19. Hapa utajifunza maisha ya Mtume kabla ya utume.
Soma Zaidi...Tofauti kat ya sura za Maka na Madina
Sura za Makka na Madina Kutokana na historia ya kushuka kwake sura za Qur-an zimegawanywa katika makundi mawili - sura za Makka na sura za Madina.
Soma Zaidi...Je Qur-an ilikusanywa na kuandikwa katika msahafu wakati wa uongozi wa Abu-Bakr(r.a)
Je Qur-an ilikusanywa na kuandikwa katika msahafu wakati wa uongozi wa Abu-Bakr(r.
Soma Zaidi...ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN
ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.
Soma Zaidi...