KISA CHA TEMBO KATIKA QURAN, KUHUSU ABRAHA KUTAKA KUVUNJA AL-KABA NYUMBBA YA aLLAH

KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji.

KISA CHA TEMBO KATIKA QURAN, KUHUSU ABRAHA KUTAKA KUVUNJA AL-KABA NYUMBBA YA aLLAH


KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBO
Tukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-ka’aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)

Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.

Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo San’a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.

Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.

Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 5739

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Sababu za kushuka surat al humazah

Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka.

Soma Zaidi...
Je, mtu anaweza kusoma quran akiwa amelala?

Kusoma Qur'an kuna faida kubwa kwa Muislamu, kwanza kunampatia thawabu, kunatoa nuru maisha yake, mwili wake na kumlinda na mashetani na watu wabaya. Quran ni dawa na pozo kwa magonjwa. Thawabu za Qur-an hulipwa kwa kila herufi. Quran pia huja kutet

Soma Zaidi...
Tofauti kati ya sura za makkah na madinah

Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Quran

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Adabu za kusikiliza quran

ADABU ZA KUSIKILIZA QURANI 1.

Soma Zaidi...
Aasbab Nuzul surat Ash sharh: sababu za kushuka alam nashrah (surat Ash sharh)

Makala hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa alam nasharah yaani Surat Ash sharh.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq

Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.

Soma Zaidi...