waqfu ni misimamo ambapo msomaji wa Quran anaruhusiwa kusimama, kuhema au kumeza mate. Na ibtidai ni kuanza baada ya kutoka kwenye waqf
HUKUMU ZA WAQFU AL-IBTIDAI
l-Waqfu Wal-Ibtidaai – Kisimamo Na Kianzio
Msomaji si kwamba muda wote atakuwa anasoma bali, wakati mwingine anapumzika, au anasimama kidogo kumeza mate au kupumua ana atakata kabisa kusoma. Hivyo hapa kuna kauli tatu ambazo inatupasa tuzijue kabla ya kuenddelea. Kauli hizo ni;-
1.Al-waqfu: maana yake ni kisimamo nako ni kukata kusoma kwa muda wa kawaida kwa ajili ya kuvuta pumzi huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
2.Al-sakt:maana yake ni kipumziko nako ni kupumzika kwa muda kwa kiasi cha haraka mbili huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
3.Al-qatw’u;maana yake ni ukataji nako ni kusimama kusoma kwa lengo la kumaliza kusoma. Hapa inabidi mtu amalize kusoma kwake mwishoni mwa aya au sura. Na inatakikana pindi anapotaka kuendelea kusoma aanze na isti’adha
ALAMA ZA WAQFU KATIKA QURAN:
1. Alama hii(صلي) inamaanisha inajuzu kuunganisha. Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii anaweza kuunganisha maneno hayo, yaani neno la nyuma na maneno yanayofata. Hivyo hapa msomaji ana hiyari ima kuunganisha au kusimama (kufanya waqfu).
2. Alama hii (قلي) inamaanisha inajuzu kusimama.
Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii atakuwa na hiyari ya kusimama.
3. Alama hii (ج) inamaanisha inajuzu kusimama ila kwa ufupi. Yaani msomaji anapokutana na alama hii ataweza kusimama hapa, ila usimamaji wake usiwe mrefu.
4. Alama hii (م) inamaanisha kusimama kwa lazima. Yaani msomaji anapokutana na alama hii kusimama kwake ni kwa lazima.
5. Alama hii (لا) inamaanisha hairuhusiwi kusimama sehemu hii. Hii inamaanisha msomaji hatakiwi kusimama pindi anapokutana na alama hii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Kwa kuwa hakuna sababu mwalumu ikiyonukuliwa kuwa ndio chanzo cha kushushwa suravhii. Basi post hii itakujuza mambo ambayo huwenda hukuyajuwa kuhusu fadhika za surabhii na mengineyo.
Soma Zaidi...Sura hii iliposhuka ilikuwa kama imekuja kuwasuta Wanafiki waliokuwa wakizungumzahabari za uongo kuhusu jeshi alilolituma Mtume wa Allah.
Soma Zaidi...Tarqiq ni kuisoma herufi kwa kuipa wepesi na tqfkhim ni kuisoma herufi kwa kuipa uzito.
Soma Zaidi...