Wanaadamu kushindwa Kuandika Kitabu Mithili ya Qur-an:

Wanaadamu kushindwa Kuandika Kitabu Mithili ya Qur-an:

(ix)Wanaadamu kushindwa Kuandika Kitabu Mithili ya Qur-an:



Ushahidi mkubwa na wa uwazi zaidi ni hii changa moto iliyonadiwa kwa wanaadamu wote katika Qur-an yenyewe. Ni kwamba, watu waliokufuru wa nyakati zote za historia ya Qur-an wanadai kuwa Qur-an si kitabu cha Allah(s.w) bali ni kitabu kinachotokana na kazi ya mwanaadamu, hususan Mtume Muhammad (s.a.w). Baadhi ya madai yao tumeshayaona katika kurasa za nyuma.


Baada ya kutoa madai yao haya yasiyo na ushahidi wowote au fununu yoyote ya ukweli, Allah (s.w), aliye Mjuzi na Mwingi wa hekima, Alitoa changamoto si kwa hawa wapinzani tu bali kwa wanaadamu wote ili baada ya hapo kila mwenye akili timamu ashuhudie kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w). Allah (s.w) alitoa wito kwa wapinzani wote wa Qur-an kuwa wakusanyike pamoja na washirikiane na wataalamu wote wa ulimwengu walio na uzoefu na uhodari katika sanaa ya uandishi kisha katika ushirikiano wao huo watoe kitabu mfano wa Qur-an. Historia nzima inatuonesha kuwa hakuna aliyefua dafu. Hebu turejee changa moto hii katika aya ifuatayo:


Sema: "Hata wakijikusanya watu (wote) na majini ili kuleta mfano wa hii Qur-an basi hawangaliweza kuleta mfano wake, hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao." (17:88)



Baada ya kushindwa kutoa kitabu mfano wa Qur-an, Allah (s.w) aliwapa makafiri tahfifu ili wazidi kutanabahi na kuhuzunika kwa kuwanadia kuwa waandike mfano wa sura kumi tu za Qur-an badala ya sura 114, kama tunavyofahamishwa katika aya ifuatayo:



Ndiyo kweli wanasema kuwa: "Ameitunga mwenyewe (Muhammad hii Qur-an)?" Sema: "Basi leteni sura kumi za uwongo zilizotungwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao (kuwaita) badala ya Allah (waje wakusaidieni kutunga hivyo) ikiwa mnasema kweli." (11:13)'



Hakuna aliyethubutu kutoa sura hizo kumi mfano wa Sura za Qur-an kwa wakati wote wa historia ya Qur-an. Allah (s.w) Mwingi wa Rehema na Mwingi wa Ujuzi na Hekima, alitoa tena tahfifu nyingine kwa kuwataka wale wote wanaodai kuwa Qur-an ni kitabu cha Mtume Muhammad (s.a.w) nao waandike angalau sura moja tu mfano wa sura za Qur-an kwa ufasaha wa lugha, mantiki, mtiririko wa maudhui na ukamilifu wa ujumbe. Hebu turejee aya zifuatazo:


"Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia mtumwa wetu, (kuwa hakuteremshiwa na Allah), basi leteni sura moja iliyofanywa na (mtu) aliye mfano wake, na muwaite miungu yenu bighairi ya Allah (wakusaidieni) ikiwa mnasema kweli." (2:23)


Je, ndiyo wanasema ameitunga? Sema: "Hebu (tungeni na nyie) mlete sura moja mfano wake na waiteni muwezao (kuwapata waje) isipokuwa Allah (wa kuwasaidieni) kama nyinyi mnasema kweli (kuwa haya ameyazua Muhammad)" (10:38)


Kama Muhammad (s.a.w) ndiye mwandishi wa Qur-an angelithubutu kweli kutoa changa moto hii kwa walimwengu wote wa nyakati zote? Mtume (s.a.w) angaliwezaje kutamka kwa uhakika kiasi hicho kuwa walimwengu wote hata wakishirkiana pamoja hawawezi kuandika kitabu mithili ya Qur-an uhakika ambao umebakia mpaka hivi leo? Kwa hiyo kushindwa kwa wanaadamu wa enzi zote za historia ya Qur-an kuleta mfano wa Qur-an angalau sura moja ni hoja tosha kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w).



Aidha Qur-an pia imewajibu wale watu wanaosema kuwa Muhammad (s.a.w) ndiye aliyeandika Qur-an kwa kuwataka watu hao wazingatie mawili: Kwanza Muhammad aliishi nao kwa muda wa miaka 40 na hakuonesha dalili zozote za kuwa mwandishi wala mshairi. Imekuwaje ghafla mtu huyo akaweza kuandika aya ambazo hakuna awezaye kuleta mfano wake? Pili, Muhammad angewezaje kuandika Qur-an na ilhali hakujua kusoma wala kuandika? Hoja hizo zinapatikana katika aya zifuatazo za Qur-an:


"Sema: Kama Allah angelitaka nisingalikusomeeni hii (Qur-an), wala asingalikujulisheni (hiyo Qur-an). Nalikaa baina yenu umri (mwingi) kabla ya haya; (hamkunisikia kusema kitu). Basi hamfahamu (kuwa haya si yangu mwenyewe kwa nafsi yangu)? (10:16)


"Na hukuwa mwenye kusoma chochote kabla ya hiki, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, (ingekuwa hivyo) wangefanya shaka wale wanaotaka kubadilisha (haki). (29:48)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 1018

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al alaqa

Asbsb nuzul surat al alaqa, sababu za kushuka surat alaqa. Sura hii imeshuka Makka na ina aya 19. Ni sura ya 96 katika mpangilio wa Quran.

Soma Zaidi...
Maswali yanayohusu quran

Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Fadhila za kusoma surat al Imran

Post hii itakufundisha fadhila na faida za kusoma surat al Imran

Soma Zaidi...
Ni nini maana ya id-gham katika hukumu za tajwid

Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake.

Soma Zaidi...
Quran na sayansi

3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran??

Soma Zaidi...
Utofauti wa Quran na hadithi Al Quds

Has utakwenda kujifunza utofauti was Hadithi Al Quds na Quran

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa surat Al-Humazah

Zijuwe sababu kuu za kushuka surat Al-Humazah katika quran

Soma Zaidi...