Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w)
Baada ya kuona madai mbali mbali yaliyotolewa kupinga kuwa Qur-an si kitabu cha Allah (s.w) na baada ya kuona udhaifu wa madai hayo, ni vyema sasa kuonesha hoja madhubuti zinazothibitisha kuwa Qur-an ni kitabu cha Allah (s.w). Katika kuthibitisha kuwa Qur-an ni kitabu cha Allah (s.w), tuna vigezo viwili
(a) Qur-an yenyewe na
(b) Historia ya kushuka kwake.
(a)Uthibitisho Kutokana na Qur-an Yenyewe:
Vipengele vinavyothibitisha kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w) kutokana na Qur-an yenyewe ni hivi vifuatavyo:
(i)Kutojua kusoma na kuandika kwa Mtume Muhammad (s.a.w).
(ii)Qur-an yenyewe inajieleza kuwa ni Kitabu cha Allah (s.w)
(iii)Hali aliyokuwa nayo Mtume katika kupokea wahyi.
(iv)Qur-an kushushwa kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka ishirini na tatu (23).
(v)Kukosolewa kwa Mtume katika Qur-an.
(vi)Kutokea kweli yale yaliyotabiriwa katika Qur-an.
(vii)Mpangilio wa Qur-an.
(viii)Maudhui ya Qur-an na mvuto wa ujumbe wake.
(ix) Wanaadamu kushindwa kuandika kitabu mithili ya Qur-an.
Hebu tuangalie jinsi kila kipengele kinavyothibitisha kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w).