Unazijua faida za kusoma Quran, na je ni faida gani utapata ukisoma Quran?
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran
1.quran ni kamba,ponyo,kinga,nuru na ni kitu chenye kuokoa.
Kwa ufupi unaweza kusema qurani ina kila kitu ambacho tunakihitajia katika maisha yetu. Qurani inaweza kutumika kama tiba ya kuondoa maradhi ana kinga dhidi ya maradhi, uadui na husda. Pia ni nuru inayoweza kumuongoza mtu wapi apite. Qurani humkinga mtu na maadui, maradhi, husda na kila kitu kubada. Maneno haya unaweza kuyakuta katika hadithi ndeefu aliyoipokea al-haakim katika mapokeza ya ‘Ablahhah Ibn Mas’ud kuwa Mtume amesema “……hakika hii qurani ni kamba ya Allah, na ni nuru iliyo wazi, na ni pozo lenye kunufaisha, na ni ngome (ya kujikinga) kwa mwenye kushikamana nayo na ni kitu chenye kuokoa kwa mwenye kuifuata.…..”
2.Qurani ni yenye kuombea shifaa siku ya qiyama.
Watu watakuwa katika hali na wakati mgumu siku ya qiyama. Katika tabu za namna hiyo qurani itakuwa ni yenye kuwaombea watu wake wapate shifaa mbele ya Allah. Amasimulia Abuu Umamah kuwa “nimemsikia Mtume akisema ‘isomeni qurani, kwani hakika itakuja siku ya kiyama hali yakuwa ni yenye kuwaombea watu wake’” (amepokea Muslin)
3.Ukisoma herufi moja unaandikiwa mema (thawabu) 10.
Amesimulia Ibn msud kuwa mtume amesema “mwenye kusoma herufi moja katika kitabu cha Allah atapata jema moja, na jema moja hulipwa kwa mara kumi kwa mfano wake.…”(amepokea Tirmidh). Katika muendelezo wa hadithi Mtume anasema ukisema ALM hizi ni herufi tatu, hivyo kila moja hulipwa kwa kumi.
4.Wenye kusoma qurani ndio watu bora.
Mtume amewapa nafasi kubwa sana watu ambao wanaisoma qurani. Katika masimulizi ya ‘Uthman Ibn ;Afan mtume amesema “mbora wenu ni yule mwenye kujifundisha qurani kisha akaifundisha.” (amepokea Bukhari, Abuu Dauw na Tirmidh).
5.Mtu atapandishwa darsa kwa kiasi alichohifadhi qurani peponi.
Watu watakapoingia peponi watapandishwa madaraja ya peponi kulingana na kiasi cha mtu anachoweza kusoma katika qurani. Amesimulia Abdallah Ibn Umar kuwa Mtume amesema ataambiwa mtu aliyeisoma qurani (akiwa peponi) soma na upande darja na uisome kama ulivyokuwa ukiisoma ulivyokuwa dunianai. Kwa hakika makazi yako yataishia pale itakapoishia aya ya mwisho utakayoisoma”. (amepokea Abuu Dawd na tirmidh).
6.Mwenye kusoma vizuri qurani atakuwa na malaika.
Amesimulia Aisha kuwa mtume amasema mwenye kusoma qurani na akawa mahiri nayo (anaisoma vizuri) atakuwa pamoja na malaika wema wenye kutii. Na yule mwenye kuisoma na akawa anakwamakwama (hajaiweza vizuri na anajitahidi aiweze) na huku anashaka atapata malipo mara mbili” (amepokea bukhari, Muslim na wengine).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Sura hii ni katika sura za kitawhidi sana. Maulamaa wanasema inatosha sura hii kuwa ni mawaidha. Imamu sharifu anasema kuwa sura hii inatosha kuwa muongozo…
Soma Zaidi...Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili
Soma Zaidi...Aina za idgham ni idgham al mutamathilain, na idgham al mutajanisain
Soma Zaidi...Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.
Soma Zaidi...Zijuwe sababu kuu za kushuka surat Al-Humazah katika quran
Soma Zaidi...SURAT AL-QURAYSH Sura hii ina majina mawili.
Soma Zaidi...Maulamaa katika elimu ya Quran wametofautiana juu ya aya ya mwisho kushuka. Hata hivyo hapa nitakutajia ambayo imependekezwa zaidi
Soma Zaidi...(x) Dai kuwa Muhammad (s.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...